DAR ES SALAAM, TANZANIA
Gazeti la Mwananchi la leo katika
habari yake iliyoongoza katika ukurasa wa kwanza, limeandika kwamba,
Sekretarieti Mpya ya CCM imepondwa kila kona, huku mmoja watu mashuhuri
waliohusishwa kuponda Sekretarieti hiyo akiwa ni Askofu Method Kilaini.
Kufuatia habari hiyo, Kilaini amekanusha habari hiyo. Nasi
tunaichapisha hapa kama tulivyoipata.
Kwa masikitiko makubwa nimesoma katika
gazeti la Mwananchi kwamba nimeiponda safu ya uongozi na sekretariati ya
CCM. Mimi sijaongea na gazeti lolote juu ya uongozi wa CCM na wala sina
nia au sababu ya kuuponda uongozi huo. Ni vibaya kwa gazeti lo lote
lile kutumia jina la mtu kwa kueneza maoni yake. Kama ni waugwana
natumaini watasahihisha waliyoyaandika. Nasikitika sana kwa walikwazwa
na hilo.
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
Askofu Method Kilaini
Bukoba Catholic Diocese
Chanzo:CCM Blog
Post a Comment