Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Abdallah Ahmad Bin Kleb amewafariji
wanachama wa Simba wa tawi Mpira Pesa waliofutiwa uanachama kwa kuwanunulia
tiketi za kwenda kuangalia mechi ya kesho ya Serengeti Boys na Kongo Brazzaville,
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Pichani Bin Kleb akipokea tiketi hizo baada ya
kuzilipia.
Picha na Bin Zubeiry.
..................
Klabu ya Simba imejikuta kwa mara nyingine ikizodolewa na mahasimu wao wakubwa Yanga baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano ya YangaSc,Bin Kleb kuwadhihaki kwa kuwanunulia tiketi za kwenda kuangalia mechi kati ya Serengeti boys na kongo akitabainisha kuwa nia yake niya kuwafariji wanachama wa kundi maarufu la Mpira Pesa waliofurushwa na Simba.
Itakumbukwa kwamba Klabu ya Yanga ilishawahi kumtoa machozi Mwenyekiti wa Simba Mhe.Rage baada ya kumsajili dakika za mwisho beki Mbuyu Twite baada ya uongozi wa Simba kujinasibu kuwazidi kete Yanga linapokuja suala la usajili wa wachezaji wa kimataifa.
Kwenye medani ya michezo Bongo hili linachukuliwa kama dongo lingine tena litakolowafanya mashabiki wa Simba kutokuwa na furaha kutokana na uongozi wao kudhihakiwa kila mara na kuonekana hawafanyi kazi kwa umakini,hali inayopelekea watani wao kuwatania nje na ndani ya uwanja.
Post a Comment