Makamu Mwenyekiti wa Chama CHa Mapibnduzi Zanzibar Dk Ali Mohammed
Shein amesema sasa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaondoka na gia mpya
katika kuimarisha na kuendeleza Chama katika ngazi zote ili kuona
kinaleta mafanikio na kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Amesema baada ya kumalizika uchaguzi wa ngazi za juu na kupata
viongozi wapya kazi iliobaki ni kuimarisha chama kuanzia shina hadi
taifa.
Amesema vikao vya chama ndivyo vinavyoimarisha na kuhuwisha chama
kwani katika vikao hivyo ndimo mnamojadiliwa na kupangwa mambo yote ya
kuendeleza chama.
Dk Shein alitoa kauli hiyo leo jioni huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
alipokuwa akizungumza na wazee wa chama hicho mara baada ya kuwasili
Zanzibar kutoka Dodoma kuhudhuria Mkutano Mkuu wa chama ambako
alichaguliwa kuwa makamo wa Mwenyekiti wa CCM upande wa Zanzibar.
Amesema chama kitaendelea kuwaenzi wazee na kutumia busara zao katika
kujenga uimara wa chama hicho na pia kupata hekima katika kukiendeleza
na kukiimarisha ili kiendelee kuwa chama chenye misingi imara na
kisichoyumba katika utekelezaji wa majukumu yake.
Hivyo aliwashukuru kwa jitihada zao za kukilinda na kukienzi chama
hicho na pia kumchagua yeye kukiongoza katika kipindi cha miaka mitano
ijayo.
Ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na wazee hao katika kukiendeleza chama cha mapinduzi.
Akizungumzia suala la utoaji maoni juu ya katiba mpya , Dk Ali
Mohammed Shein amefahamisha kuwa nia ya kuwepokuraya maoni ni kuimarisha
muungano na sio kuvunja, hiyo ndio sera ya chama cha mapinduzi.
Ameongeza kuwa katika mapendekezo hayo hapana pahali palipoandikwa au
kusema kwamba Muungano uvunjwe. CCM ina sera yake ya kuimarisha muundo
wa serikali mbili na sio vyenginevyo. Sera ya ccm iko wazi maelezo yake
yapo wazi alisisitiza Dk Shein.
Amesema watu wamekuwa wakitia chumvi juu ya suala hili hivyo si vyema
kuwafuata kwani sisi tunasera yetu (CCM) na wao wanasera zao, sisi tuna
chama chetu na wao wana vyao.
Alifahamsha kwamba chama ndio kiwe mbele na hakuna wa kuwababaisha
wana ccm, kwani chama ndio kilichodhibiti nchi ibakie katika mikono ya
wazalendo wa Tanzania si vyenginevyo.
Alitahadharisha kwamba wapo watu bado wanaitaka Zanzibar na kama wana
ccm hatukuwa makini na tukafanya mchezo watu wataichukuwa nchi.
Kuhusu amani na utulivu wanchi, Makamo mwenyekiti huyo alisema bado
wako watu wanaichezea amani iliopo jambo ambalo ni hatari sana.Serikali
haitavumia kuona amani inachezewa.
Alivipongeza vikosi vya ulinzi na usalama kwa kurejesha utulivu na kuendelea kulinda maisha namaliza raia.
Amerejea kauli yake kwamba serikali haiwezi kuvumilia tena vitendo
vinavyofanywa na Muwamsho na kusema kwamba serikali itaendelea kuchukua
hatua za kisheria kwa kikundi chochote ambacho kitaashiria uvunjifu wa
amani hapa nchini.na
kamwe serikali haitovumilia kuchezewa.
Haturudi nyuma katika kulinda
amani ya zaznibar ili sifa nzuri ya visiwa hivi isiondolewe.
Nao wazee wa CCM wa Mikoa mitatu ya Unguja walitoa pongezi zao kwa
Mkutano Mkuu wa Taifa na Ushindi wa asilimia miamoja (100%)kwa Dk shein
na kusema kwamba hivi sasa chama kimeingia katika muelekeo wa uhakika
zaidi wa kukipatia ushindi wa kishindo chama hicho kwenye uchaguzi mkuu
ujao. Kwani kutokana na sababu za kiitikadi kilichojitokeza ni kuzorota
kwa utendaji katika chama hasa ngazi za chini katika kipindi kilichopita
cha uongozi.
Wamesema sikweli maneno yaliosemwa na kiongozi mmoja wa kisiasa kamba
doria zinazofanywa na askari kwa lengo la kudumisha amani vinafanya
doria katika maeneo yenye wafuasi wa chama hicho na eti kwamba
kinawabughudhi.
Waliwataka viongozi wa juu kukumbushana umuhimu wa kujikinga na fitna na kuziepuka taarifa za kubuniwa.
Chanzo: http://www.mzalendo.net/habari
Post a Comment