Mbunge
wa Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari akiwa kwenye gari ya wazi na
wafuasi wa Chadema katika mji wa Usa River wakifurahia matokeo ya
uchaguzi kuwatafuta wenyeviti wa Serikali za mitaa ambapo Chadema
waliweza kuibuka kidedea kwa kujinyakulia uongozi wa mitaa 6 kati ya
tisa iliyokuwa inagombaniwa.
Shamrashamra za kushangilia ushindi
Mh
Joshua Nassari akipokea matokeo ya awali kutoka vituo mbalimbali vya
kupigia kura ndani ya Halmashauri ya mji mdogo wa Usa River kwa njia ya
simu ndani ya kituo cha chama chake cha kufanya majumuisho ya kura kwa
upande wa Chadema jana.
Hali ya barabara ilikuwa ni ya utelezi na matope sana kwa meoneo mengi ya mji
Mh
Nassari akifurahia matokeo yaliyokipatia ushindi chama chake na baadhi
ya viongozi wa chama na wadau wengine mahali walipojibanza barazani
kukwepa mvua
Hapa
Nassari alikuwa akiwafahamisha wananchi matokeo rasmi ya uchaguzi ambao
walishiriki, baada ya kupata matokeo ya maeneo yote.
Gari iliyotolewa na mmoja wa madiwani wa Chadema mjini Arusha ili kusaidia kampeni hizo zilizopelekea CHADEMA kuipiga kumbo CCM
Kabla
ya matokeo ya jumla, CCM nao walionekana mitaani wakipita kwa
shamrashamra kuanza kushangilia lakini furaha yao ilizimwa ghafla na
matokeo ya mwisho baada ya kujikuta wameambulia mitaa 3 tu kati ya 9.
Katika uchaguzi huo uliofanyika jana huku
mvua kubwa ikinyesha maeneo tofauti kiasi cha kuharibu mawasiliano kwa
baadhi ya maeneo, ulishirikisha jumla ya vyama vitatu ambavyo ni
CHADEMA, CCM na AFP ambao walishiriki mitaa miwili tu.
Kwa
matokeo hayo ya viti sita kwenda CHADEMA, ni wazi kuwa nafasi ya
kuongoza Halmashauri ya Mji mdogo wa Usa River itachukuliwa na chama
hicho kwa maana kwamba tayari wanakura nyingi endapo kila chama
kitapigia upande wake! Viti maalumu pia vinaweza kuongeza idadi ya kura
za Chadema katika kumchagua meya wa Halmashauri ya Mji huo mdogo wa Usa
River.
Chadema waliibuka washindi kwa kuchukua uenyekiti wa mitaa ya Mji Mwema, Kisambale, Manayata Kati na Banana.
Mitaa mingine ni Magadini na Ngarasero ambao ulielezwa kuwa ngome kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM katika mji huo.
CCM kwa upande wao waliweza kujinyakulia mitaa ya Mlima Sioni, Magadirisho na Usa Madukani.
Chanzo Noise of Silence Blog.
Post a Comment