
Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Wilbrod Slaa
--
 Na Edson Kamukara
SIKU
 moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuwataka
 makada wa chama hicho kujibu mapigo ya wapinzani,akidai wanafanya kazi
 ya kueneza uongo na kupotosha wananchi, CHADEMA imesema inamvutia pumzi
 kabla ya kumjibu.
Akihitimisha
 mkutano mkuu wa CCM mjini Dodoma juzi usiku, Rais Kikwete aliwataka 
mawaziri na makada wa chama hicho kufanya mikutano ya hadhara na kutumia
 vyombo vya habari kujibu hoja za wapinzani badala ya kutegemea nguvu za
 Jeshi la Polisi.Huku
 akionekana kukasirishwa na kasi ya CHADEMA, Rais Kikwete alimtaja wazi 
wazi Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, kuwa aliwahi 
kumzulia uongo pamoja na mwanaye Ridhiwani.
“Slaa
 aliita mkutano akasema mimi, mwanangu Ridhiwani na Rostam Aziz 
tulikutana kwenye hoteli moja jijini Mwanza, huku akijua siku aliyoitaja
 mi nilikuwa kusini nikiendelea na shughuli zangu,”alisema.
Rais
 Kikwete alisisitiza kuwa hiyo ndiyo kazi ya upinzani,watu wazima 
hovyo,wanasema uongo mbele wananchi na hata wakati mwingine kwenye 
vyombo vya habari wakinukuu takwimu za uzushi.
Alipoulizwa
 jana kuhusu madai hayo ya kueneza uongo kwa wananchi,Dk.Slaa alicheka kisha akasema:“Tunawatafakari na tutawajibu,ila siyo
 leo, wala hatuna haraka.“Mimi
 kwa kweli sikusikiliza hotuba yake, na hata mkutano wa CCM 
sijaufuatilia, ila kama Kikwete kasema hayo unayoniuliza, basi tutamjibu
 kwa utaratibu rasmi wa chama, leo sisemi kitu.
“Sisi
 ni watu makini, tunaamini katika kile tunachokisema wala wasipaniki, 
tutawajibu.Maana wanadhani tunapoteza muda kufuatilia mkutano wao,nilimsikia hata Nape Nnauye akisema juzi kuwa anajua tumeacha kazi 
tunawakodolea macho,”alisema.
Dk.Slaa alisema kauli ya Nape ambaye pia
 ni Katibu wa Halmashauri Kuu(NEC),Itikadi na Uenezi wa CCM,inachekesha,
 kwani CCM ya wao kuacha 
kazi zao na kuikodolea macho ilikuwa ya zamani si hii ya leo.
Katika
 kile kinachoonekana kama CHADEMA kuinyima usingizi serikali na CCM, 
Kikwete aliagiza mawaziri wote kujiwekea utaratibu wa kila mmoja kutoa 
taarifa za utekelezaji wa majukumu ya serikali katika vyombo vyote vya 
habari.Alisema
 kwa vile viongozi wa chama na serikali hawajibu taarifa za upotoshaji 
zinazotolewa na wapinzani, wananchi wanapozisikia zikirudiwa rudiwa bila
 kukanushwa wanaziamini.
Chanzo:Haki Ngowi. 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Post a Comment