Mkuu
wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Daudi Ntibenda akizungumza na wajumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) jana jumatatu Novemba 19, 2012 wakati
wajumbe hao walipofika ofisini hapo kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni
ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani humo. Kushoto ni mjumbe wa Tume, Bi.
Mwantumu Malale.
Akina
Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha
wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya
ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo jana
jumatatu Novemba 19, 2012
Mjumbe
wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati
jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa
wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha
Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa
kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana
jumatatu Novemba 19, 2012.
Post a Comment