Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BAADA YA NGASA KUUZWA SIMBA WALILIA FEDHA ZAO

Hans Poppe

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
SIMBA SC imesema haitaki ugomvi wala malumbano na Azam FC, bali wanataka warudishwe fedha zao zote walizotoa kumsaini mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa, Sh. Milioni 55 pamoja na faida juu.
 
Azam FC jana imemuuza Mrisho Khalfan Ngassa kwa dola za Kimarekani 75,000 (Sh. Milioni 120) kwenda El Merreikh ya Sudan ambako amesaini mkataba wa miaka miwili, utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa dola za Kimarekani 4,000 (Sh Milioni 6,) kwa mwezi huku naye akilipwa dola 50,000 (Sh. Milioni 75) za kusaini.
 
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kwa simu jana kutoka Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba wao walimsajili mchezaji huyo kwa taratibu, ila wanashangaa sasa Azam wanataka kufanya mambo kinyume cha utaratibu.
 
“Sisi tuna mkataba na huyu mchezaji, ambao tulisaini na wao Azam, ambao ilikuwa kama kuununua mkataba wake wa kule Azam, baada ya wao wenyewe kushindwana na huyo mchezaji. Tuliwapa Sh. Milioni 25 na baadaye tukaongeza naye mchezaji mkataba wa mwaka mmoja, tukampa Sh. Milioni 30,”alisema Hans Poppe.  
 
Kapteni huyo Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), alisema kwa kuwa hawataki malumbano na Azam, wanaomba warejeshewe fedha zao na faida kidogo, kwani mchezaji huyo amenunuliwa akiwa anachezea Simba SC.
 
 
Awali, Merreikh walitaka kumpa mkataba wa miaka mitatu Ngassa wenye thamani ya dola 100,000, lakini wakala wake Alhaj Yussuf Said Bakhresa akakataa akisema utambana mchezaji wake aking’ara na kutakiwa na klabu nyingine.
 
Sasa, Ngassa baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge mwishoni mwa wiki hii, atakwenda Sudan kufanyiwa vipimo tayari kujiunga na klabu hiyo, ambayo ni jambo la kawaida kucheza hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika.
 
Azam walimtoa kwa mkopo Ngassa mwanzoni mwa Agosti, mwaka huu baada ya kukerwa na kitendo cha mchezaji huyo kubusu jezi ya timu yake ya zamani, Yanga, katika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
 
Alifanya hivyo, baada ya kufunga bao la ushindi akitokea benchi na kuiwezesha Azam kutinga fainali ya michuano hiyo, ambako walifungwa na Yanga 2-0, naye kwa mara nyingine akitokea benchi na kushindwa kufunga, hivyo kutuhumiwa kucheza kinazi.
 
Ilielezwa kwamba Simba walitoa Sh. Milioni 25 kumnunua kwa mkopo mchezaji huyo, ingawa baadaye Simba wakasema waliununua mkataba wa mwaka mmoja aliobakiza mchezaji huyo Azam FC, nao wakamuongezea wa mwaka mmoja kwa kumsainisha kwa Sh. Milioni 30, kati ya hizo Milioni 12 akipewa taslimu na 18 
 
Chanzo:Bongo Staz
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top