Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula
ALIYEKUWA Mbunge wa Njombe Magharibi (CCM), Yono Kevela
amemtuhumu Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula kwa kuvuruga uchaguzi
wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya chama hicho, Wilaya ya
Wanging’ombe kwa kuwabeba baadhi ya wagombea.
Katika madai yake ambayo ameyakatia rufani, Kevela amesema katika uchaguzi huo uliofanyika Julai 29 mwaka huu, mbali na kuwabeba wagombea hao, Mangula alishiriki kutengeneza makundi ya vitisho, rushwa na lugha za kejeli dhidi yake.

Alisema siku ya uchaguzi akiwa amekaa meza kuu,
Mangula alipopewa nafasi ya kuhutubia, aliwaambia wajumbe kuhakikisha
Kevela na mgombea mwingine Hamisi Nurdin hawapiti.
“Mangula alisema watu hao wasichaguliwe kwa kuwa
wana malengo tofauti na yale ya kukitumikia chama,” alidai Kevela.
Malengo yaliyodaiwa katika rufani hiyo ni kuwa Kevela anautaka ubunge wa
Njombe Magharibi na Nurdin ana nia ya kutaka Makao Makuu ya Wilaya ya
Wanging’ombe yawe Igwachanya.
Rufani hiyo imetaja tuhuma nyingine dhidi ya
Mangula kuwa ni timu yake kutangaza kuwa Kevela amejitoa kwenye
uchaguzi… “Hili liliathiri pia ushindi wangu katika uchaguzi huo.”
Rufani hiyo ya Kevela nakala yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CCM, Idara ya Usalama na Maadili ya CCM, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.
Rufani hiyo ya Kevela nakala yake imepelekwa kwa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa CCM, Idara ya Usalama na Maadili ya CCM, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa chama hicho na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe.
Kevela katika rufaa yake hiyo, anataka matokeo ya
uchaguzi huo yafutwe kwa kuwa ulikiuka vifungu kadhaa vya kanuni
kikiwamo cha Miiko ya Shughuli za Uchaguzi na Uteuzi wa wagombea ukurasa
wa 39, cha Kanuni za Uteuzi toleo la Februari 2010, Kifungu namba 22
(1-6). Hata hivyo, pamoja na kukata rufani hiyo, Kevela amesema ana
shaka kwamba haki itatendeka kwani, mtu anayemlalamikia ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, ambayo kulingana na Kanuni
za Uchaguzi za CCM, ndiyo itakayopitia malalamiko hayo na kuyatolea
uamuzi.
Kamati hiyo inatakiwa iwe imekamilisha kazi yake ndani ya miezi sita na Mangula alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo dhidi yake alisema hazijamfikia na wala hazijui.
Kamati hiyo inatakiwa iwe imekamilisha kazi yake ndani ya miezi sita na Mangula alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo dhidi yake alisema hazijamfikia na wala hazijui.
“Hayo hayajanifikia na siyajui. Hata hiyo rufaa
haiji kwangu. Malalamiko yote yanashughulikiwa na jopo la wataalamu
kabla ya kufikishwa kwetu. Hivi sasa malalamiko yote yako katika hatua
ya uchambuzi na kimsingi yatakayoshughulikiwa ni yale yanayohusu rushwa
pekee.”
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipotakiwa
kutoa ufafanuzi kuhusu madai hayo alisema asingeweza kufanya hivyo kwa
kuwa alikuwa na siku chache tangu alipoanza kazi hiyo na kutaka aulizwe
Katibu wake wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Alipoulizwa, Nape alimtaka mrufani kutokuwa na
wasiwasi juu ya kutendewa haki akisema kwa kawaida rufani hazisikilizwi
na mtu mmoja.
Alisema baada ya kuchambuliwa, rufani zote
zinafikishwa katika kikao cha sekretarieti ambayo huzipitia na
kuzipeleka katika Kamati ya Usalama na Maadili kisha Kamati Kuu na yapo
ambayo huishia katika ngazi hiyo na mengine kupelekwa hadi Halmashauri
Kuu kwa hatua zaidi.
Nape alisisitiza kuwa hakuna uamuzi utakaofanywa
na mtu mmoja … “Labda aseme (Kevela), kuwa hana imani na Kamati Kuu ya
chama chake na hapo ndipo labda tutaangalia kanuni zinasemaje lakini kwa
sasa hali halisi ndiyo hiyo,” alisema.
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment