Vilabu vya Ligi ya soka ya Ujerumani - Bundesliga vimekubali mpango wa
hatua za kuimarisha usalama viwanjani kutokana na shinikizo la kisiasa
kufuatia ongezeko la ghasia za mashabiki.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwakagua vilivyo mashabiki katika
michuano mikubwa, kuondoa kabisa matumizi ya fataki ambazo tayari
zimepigwa marufuku na kuwapa adhabu kali kwa wale watakaokiuka sheria
hizo.
Sheria hizo zimezusha tetesi kutoka baadhi ya makundi ya mashabiki yenye
wasiwasi kwamba vilabu vinalenga hasa kuondoa utamaduni maarufu wa
masbahiki kusimama viwanjani katika soka ya vilabu Ujerumani. Hata Hivyo
maafisa wa Ligi wamekanusha madai hayo.
Huub Stevesn ahakikishwia kazi yake
Kwingineko Mkufunzi wa klabu ya Schalke 04 Huub Stevens amehakikishiwa
kuwa atasalia katika uongozi wa klabu hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya,
hata baada ya mchuano wa mwisho mwaka huu dhidi ya Freiburg leo
Jumamosi, na licha ya matokeo duni katika mechi za karibuni.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu Horst Heldt amesema klabu hiyo itaendelea
kuwa na utulivu wakati ikijadili masuala hayo yote. Heldt amesema mambo
yatakuwa mazuri tena na wataanza kusjaili ushindi. Schalke wamepoteza
mechi zake tatu za mwisho na hawajashinda hata moja kati ya mechi tano
na kusonga nafasi ya tano katika Bundesliga.
Schalke ambao pia wako katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho
wiki ijayo, wamefuzu katika awamu ya 16 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa
kumaliza wa kwanza katika kundi lao.
Wakati huo huo, kiungo wa Schalke Jermaine Jones amepigwa marufuku
kushiri mechi nne za Bundesliga baada ya kufurushwa uwanjani katika
mchuano wa wiki iliyopita walioshioshindwa magoli matatu kwa moja na
Stuttgart. Jones anashikilia rekodi ya klabu hiyo kwa kufurushwa
uwanjani mara tano.
Löw aridhika na matokeo ya vilabu vya Bundesliga
Mkufunzi wa timu ya kandanda ya Ujerumani maarufu kama Die Mannshaft
Joachim Löw amesema rekodi ya timu saba za Bundesliga kufuzu katika
awamu ya mwondowano katika Champions League na Europa League, inapaswa
kuisaidia timu ya taifa ya Ujerumani kupata mafanikio barani Ulaya. Löw
amesema yamekuwa matarajio yake kwamba Ujerumani iwe na timu nyingi
katika awamu ya mwondowano na siyo Bayern pekee. Amesema ni muhimu kwa
wachezaji kupata ujuzi, na kutengeneza msingi imara kwa mwaka ujao.
Kwa mara ya kwanza vilabu saba vya Ujerumani vitashiriki katika awamu ya
mwondowano katika Ligi ya Mabingwa na pia Europa, wakati droo
itakapofanywa katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Ulaya UEFA mjini
Nyon, Uswisi mnamo Desemba 20.
Bayern Munich, Borussia Dortmund na Schalke 04 viko katika Ligi ya
Mabingwa wakati Bayer Leverkusen, Hanover 96, VFB Stuttgart na Borussia
Moenchengladbach vikishiriki katika awamu ya 32 ya Ligi ya Europa.
Ujerumani wako kileleni mwa kundi lao la kufuzu katika dimba la dunia
mwaka wa 2014 nchini Brazil na uongozi wa tofauti ya pointi tatu mbele
ya nambari mbili Sweden ambao hawajacheza mchuano mmoja.
Ujerumani inacheza mchuano wake wa kwanza wa kimataifa mwaka wa 2013
dhidi ya Ufaransa mjini Paris mnamo Februari sita katika mchuano wa
kirafiki, kasha wapambane na Kazakhstan nyumbani na ugenini katika mechi
za kufuzu kwa dimba la dunia mwezi Machi.
Post a Comment