*Mkutano wa CCM wavurugika, watu wajeruhiwa, polisi waingilia kati
*Mangula, Dk. Mwakyembe waonja joto, warushiwa chupa za majiVURUGU kubwa zimezuka na kusababisha baadhi ya watu kujeruhiwa vibaya, baada ya kutokea mapambano baina ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Vurugu hizo zilisabaishwa kufungwa kwa muda kwa baadhi ya barabara, baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philiph Mangula na Mawaziri Dk. Harrison Mwakyembe na Jerryson Lwenge.
Wafuasi wa Chadema baada ya kuona hali ya usalama imedhibitiwa ndani ya Uwanja wa Nyamagana kulikokuwa kukifanyika mkutano wa hadhara, waliamua kuwasubiri viongozi wa CCM pamoja na wafuasi wao katika makutano ya Barabara za Kenyatta na Posta katika mzunguko wa magari na walianza kuwazomea kwa kuwaita mafisadi, huku wakiwatupia chupa za maji pamoja na mawe.
Kutokana na vurugu hizo, vijana wa CCM walianza kuwatimua wafuasi hao wa Chadema kwa kupambana nao hali iliyozusha vurugu kubwa na watu kadhaa kujeruhiwa vibaya kutokana na kupigwa mawe pamoja na fimbo.
Kutokana na vurugu hizo, Jeshi la Polisi liliwatawanya wafuasi wa vyama hivyo na kuwachukua majeruhi zaidi ya 10 na kuondoka nao.
Kutawanywa kwa vijana hao kuliwafanya wanachama wa CCM waliokwama katika Uwanja wa Nyamagana kuweza kutoka kwa kutumia mabasi maalumu waliyokuwa wameandaliwa kuwarejesha makwao.
Akihutubia mkutano huo, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Mwakyembe, aliapa kuendelea kuwasafisha viongozi wasio waaminifu walioko katika taasisi zilizo chini ya wizara yake na kusema ambao hawataki kubadilika wanapaswa wajiondoe wao wenyewe.
“Nitawafyeka wote ambao wamekuwa wakishindwa kubadilika na kuchuma mali za wananchi bila huruma, wapo ambao najua watanuna na wamekuwa wakitishia kuhamia vyama vya upinzani, waende tu kwani hawatufai.
“Kuna baadhi waliamua kwa makusudi kuchomoa baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kumsaidia mgeni ainyonye nchi hii, ufisadi umekithiri na nitaendelea kupambana nao kwa kuwa tayari nimeshachukua kwa kufanya mabadiliko katika baadhi ya maeneo muhimu yaliyo chini ya wizara,” alisema Dk. Mwakyembe.
Kwa upande wake, Meya wa Ilemela (Chadema), Henry Matata, alisema yuko tayari kuisambaratisha Chadema na tayari ameshaanza kwa kuwatimua madiwani wa chama hicho kwa kutumia rungu lake la Umeya.
“Mimi ni diwani wa Mahakama nimechaguliwa na madiwani wa CCM, hivyo CCM ni nyumbani kwangu na niko tayari kuwasaidia waweze kuchukua nafasi ya udiwani katika kata ambazo niliwatimua madiwani wa Chadema kutokana na kushindwa kuhudhuria katika vikao kwa mujibu wa sheria na kanuni,” alisema Matata.

CHANZO:MTANZANIA
Post a Comment