BUNGE linatarajia kufuta utaratibu wa
kurusha matangazo ya moja kwamoja kupitia televisheni kwa madai ya
kukomesha vitendo vya baadhi ya wabunge kukiuka kanuni za bunge na
kuleta vurugu kwa kutafuta umaarufu bila kujua kwamba tabia hiyo inaleta
picha mbaya katika jamii.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Bunge
Dk.Thomas Kashilila jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya
mapendekezo ya kuanzisha kamati ya bajeti na kuvunjwa kwa baadhi ya
kamati za bunge.
Amesema kuwa ili kuleta maadili kwa
baadhi ya wabunge ambao wamekuwa wanashindwa kufuata kanuni za bunge na
kutumia nafasi hiyo kwa kutafuta umaarufu kwa sasa wameomba kufutwa
utaratibu wa kurusha matangazo ya bunge ya moja kwa moja badala yake
watarekodi ili kuondoa hoja zisizokuwa za msingi.
Ameongeza kuwa kuna idadi kubwa ya
wabunge wamekuwa wakikiuka kanuni za bunge makusudi na kusababisha
kuleta vurugu bungeni wakati jamii ikiendelea kutazama mabishano
yasiyokuwa na hoja za msingi.
Dk Kashilila amesema kuwa kwa sasa kuna
baadhi ya kamati za bunge ambazo zimevunjwa kutokana na baadhi ya kamati
hizo kuingilia katika utendaji jambo ambalo limekuwa likipoteza maana
ya kamati hizo.
Hivi karibuni baadhi ya kamati ikiwemo
ile ya Mashirika ya umma POAC zimefutwa na kuacha maswali mengi kwa
baadhi ya wananchi juu ya hatua hiyo.
Fuatilia mjadala na maoni juu ya hili kwa kubonyeza hapa
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/400713-bunge-kusitisha-kurusha-vikao-vyake.html
Post a Comment