Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

DIAMOND PLATINUM:MAMA YANGU NDIYE MGANGA WANGU



Diamond akipata baraka za mama yake
Huenda ile story ya kwamba Diamond amepata na anaendelea kupata mafanikio kutokana na kutumia waganga wa kienyeji si kweli!! You never know! Staa huyu ambaye gazeti la Daily Nation limemtaja kuwa miongoni mwa wasanii wa Bongo Flava matajiri zaidi, yupo karibu mno na mama yake mzazi na pengine ndio maana anafanikiwa, nani kama Mama? Vipi kama mafanikio yake ni thawabu halisi kutoka kwa Mwenyezi Mungu?

Akipiga stori na thesuperstarstz diamond amesema kuwa yeye ana mtegemea mungu na katika dunia nguzo yake pekee ni mama yake mzazi hivyo kama kuna swala la mganga basi mama yangu ndio mganga wangu kwani haniruhusu kutoka hadi tumefanya dua kumshukuru mungu,msanii huyo aliendelea kuchonga na thesuper starstz kuwa hawezi kufanya jambo bila mama yake na hata akitaka kutoka ni lazima apate dua na baraka za mama yake mzazi na ndio maana anafanikiwa sana msanii huyo ambaye anatajwa sana katika vyombo vya habari amesema anamuamini mungu na ndio maana hawezi kupoteza hata dakika moja bila kumuomba mungu.

The super stars tz ilifunga safari hadi nyumbani kwa diamond maeneo ya sinza mori na kuongea na bi mkubwa huyo ambaye alianza kwa kusema,,,Namshukuru mungu kwa kunipa afya pia na mshukuru kwakuzidi kumuangazia mwanangu Nasibu katika kazi zake alisema mama huyo,na alipoulizwa kuhusu kashfa zinazomkabili mwanae mama huyo amesema kuwa si za kweli na ana muamini sana mwanae na hajamlea katika mazingira hayo alimaliza mama huyo.

Hizi ni picha ambazo Diamond ameziweka kwenye website yake na kuandika kwenye moja ya picha hizo: Siku zote kabla ya kwenda popote lazima tupitie kwa mama yetu mpendwa atupe Barka zake na nyingine hiyo juu akiandika: Nikipokea baraka za Mama ….Nijaliwe Mema….na Niende kwa Amani…!!

 
Wasafi wakipata baraka za mama


Diamond akisalimiana na mashabiki wake
The super stars tz inazidi kumpongeza kijana Diamond kwa kazi nzuri na kumuombea mungu aendelee kumjalia katika kazi zake pia inawaomba wadau haswa watanzania tuthamini vya kwetu tusiwe watu wakuongea na kutafuta mabaya ndio tuyaseme kijana anajitaidi basi tumuunge mkono ili afike kama akina jiga ,50 na wengine tunao waona na kuwasikia huko kwa wenzetu. 
 
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top