Leodegar Tenga; Rais wa TFF
.............
Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepokea barua ya Serikali ikielezea uamuzi wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Dk. Fenella Mukangara kutengua uamuzi wa Msajili wa Klabu na Vyama vyaMichezo nchini kuidhinisha marekebisho ya Katiba ya TFF toleo la 2012.Baada ya kupokea barua hiyo jana alasiri (Februari 25 mwaka huu).
Kutokana na barua hiyo ya Waziri wa habri, vijana , utamaduni na Michezo Sekretarieti iliwasiliana na Rais wa TFF, Leodegar Tenga ambaye ameagiza kuitishwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji kujadili tamko hilo.
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya TFF ambacho kitafanyika Jumamosi (Machi 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.Kinatazamiwa kutoa tamko litakalo toa mwanga ya sintofahamu iliyogubika uchaguzi huo wa TFF hasa baada ya serikali kuingilia kati.
Kuingilia huko kwa Serikali kulitokana na utata juu ya kuenguliwa kwa baadhi ya wagombea kiasi cha kumbakisha mgombea mmoja katika nafasi ya Rais wa TFF na wadau kuhoji inakuwaje mgombea Jamal Malinzi aliyeshiriki uchaguzi uliomuingiza madarakani Rais wa sasa Tenga leo akose sifa ilihali mwanzoni alishiriki uchaguzi.
Pia Serikali imeamua kuingilia kati sakata hili la uchaguzi wa TFF na kuamuru kufutwa kwa katiba ya sasa ya Shirikisho la soka na itumike katiba ya mwaka 2006 hii ni kutokana na kasoro nyingi zilizopo kwa katiba ya sasa.
Wizara ya Habari, utamaduni ,vijana na Michezo jana ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikieleza mapungufu hayo na kusema katiba ya sasa si halali,kwani msajili wa vyama vya michezo aliyedaiwa kuipitisha katiba hiyo ameondolewa.
Sakata hili lilichochewa na Kamati ya Rufani ya TFF chini ya Iddi Mtiginjola pale ilipowaengua kina Malinzi na kumuacha Makamu wa sasa, Athumani Nyamlani kuwa mgombea pekee katika nafasi ya Urais wa TFF.
Pamoja na Serikali kuingilia kati tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilishaupiga stop uchaguzi huo kutokana na malumbano yaliyotokea na wameshaanza uchunguzi kujua kiini cha matatizo hayo.
NA Chediel
Post a Comment