Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MTATIRO:JOB NDUNGAI HAJAKOSEA, ANAENDELEZA ALICHOTUMWA.

Ndiyo maana tunasisitiza kwamba kwenye KATIBA mpya tuangalie utaratibu wetu wa namna ya kumpata spika na naibu spika. Kama hatufanyi hivyo maspika wetu lazima waendeleze umbumbumbu wa kuitetea CCM iliyochoka, kuchakaa na sasa inatafuta nani imfie, kila mwana CCM anajua itakufa, kina ndungai na makinda wanachofanya ni kukwepa isifie mikononi mwao.

Mchezo huu wa mechi ya simba na yanga kuamuliwa na refa ambaye ni mshabiki na mwanachama wa simba au yanga unatugharimu katika kila eneo. Ukienda hata kwa tume ya taifa ya uchaguzi ati inateuliwa na mwenyekiti wa CCM halafu eti tunategemea wateuliwa watende haki kwa vyama vya upinzani.

Mchezo huu pia uko hata kwa uteuzi wa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, nchi hii huwezi kushikilia nafasi ya KOVA na nyingine nyingi za juu za polisi kama huiungi mkono CCM. Maafisa wa juu wa polisi wenye msimamo wa kutetea wananchi wote kwa usawa hutawasikia hata siku moja wamekuwa ma-RPC n.k......

Upuuzi huu unaendelea hadi kwa jeshi la ulinzi na usalama, nako kama huishabikii CCM huwezi kuwa mtu yeyote wa maana. Utaishia kuwa ofisa wa makao makuu ya jeshi, basi. Tuna matatizo na uozo mkubwa sana kwenye mfumo wetu wa uongozi wa idara na vyombo mbalimbali vya serikali usiozingatia sifa na uwezo wa mteuliwa. Sasa tumejenga taifa ambalo ili mtu apate wadhifa muhimu sana kwa mihimili ya dola lazima kwanza alambe nyayo za CCM.

Hata ukienda huko mikoani, nyadhifa muhimu kama za ukuu wa wilaya na ukuu wa mkoa zina nguvu kubwa sana. Lakini wanaoteuliwa kushika nyadhifa hizo ATI lazima kwanza wawe makada wa CCM na watakaoitetea kwa nguvu. Mkuu wa mkoa atatendaje haki ikiwa anateuliwa tu ki-CCM ili eti akatetee wananchi wote na ambao hawakumchagua? Ni jambo lisilowezekana asilimia MIA moja. Ndiyo maana wakuu wa mikoa na wilaya kila kukicha huzalisha vurugu mahali walipo, wanasahau jukumu la kusimamia haki na wajibu wa wananchi wote kwa ujumla, wamekaa kutetea CCM tu.

Binafsi simshangai Job Ndungai wala wenzie, tatizo ni kubwa kupita hapo. Job Ndugai anatekeleza kule wanachotekeleza majaji na mahakimu mahakamani katika kesi nyingi ambazo lazima CCM ilindwe.

Job Ndungai anafanya yale wanayofanya wakuu wa vikosi vyetu vya ulinzi na usalama ili kuilinda CCM huku wakisahau kazi yao KUU ya kulinda raia na Mali zao.

Sikushangazwa na chochote kwa sababu Job Ndungai na Anna Makinda siku zote wanafanya kile wanachofanya wenzao tume ya taifa ya uchaguzi, wakuu wa mikoa na wilaya, wakurugenzi wa halmashauri na watendaji wa kata na vijiji... Ni kazi ile ile, kuilinda CCM hadi tone lao mwisho la damu. ......CCM kwanza, maslahi ya wananchi baadaye!

Na ukifuatilia asili ya majukumu ya viongozi utakuta yapo mawili makubwa. Jukumu la kwanza ni kusimamia haki na usawa kwa wananchi wote bila kujali rangi, dini, kipato, tofauti za itikadi, jinsia n.k. Na jukumu la pili ni kusimamia maadili na miongozo ya taaluma. Hizi ndizo kazi KUU mbili za viongozi kokote kule waliko.

Sasa mfumo wetu wa nchi umeoza katika eneo hili. Viongozi hawasimamii haki na usawa ili kujenga jamii yenye matumaini makubwa. Viongozi hawasimamii maadili na miongozo ya taaluma zao, hapo ndipo tunalipeleka taifa kuzimu.

Wanachosahau kina ndungai ni kwamba, hawatakuwepo madarakani milele. Wataondoka tu, na killichofanyika jana DODOMA ni kiashiria kingine sahihi kwamba CCM wamebebana weeeee hadi wamechoshana wao kwa wao. Wamekosa mbinu za kuongoza baada ya hii ya kubebana kufikia ukomo. Na bahati nzuri, wananchi wameanza kutambua kuwa serikali iliyoko madarakani iko kwa ajili ya ka-kikundi kadogo ka ma-CCM wachache wezi na mafedhuli.

Mafedhuli hawa wanaweza kukuua hadharani na bado wakajitetea, wamefanya hivyo ULIMBOKA na wamejaribu kutengeneza kiini macho, wamefanya hivyo kwa Mwangosi na wao wanaendelea kuponda raja, wanafanya hivi kila siku tena waziwazi. Wanaua hadharani na wanalindana ndani ya jamii yetu.

Kitakachotokea siku si nyingi ni anguko rasmi la CCM. Hawana hoja za kuzuia upinzani tena, sasa ni kutumia MAGUVU na kukwepa kujadili kila kitu. TUJIPANGE KUPOKEA KIFO NA MAZIKO RASMI YA CCM, NDUNGAI HAJAKOSEA .... ANAENDELEZA ALICHOTUMWA NA WATAFUNAJI WA NCHI HII.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top