Siku mbili zilizopita mshauri na
mchambuzi wa masuala ya soka la kiafrika kutoka nchini Ivory Coast
Mamadou Gaye alifanya mahojiano ya kipekee na mtandao kuhusu mambo
mbalimbali yanayohusiana na soka la Afrika, kuanzia michuano ya kufuzu
kombe la dunia ambapo nchi yake ya Ivory Coast ipo kundi moja na
Tanzania, mpaka kuhusu uchaguzi wa uraisi wa shirikisho la soka la
Afrika CAF.
Mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Watu wa Ivory Coast wameupokeaje ushindi wa Tanzania dhidi ya Morocco ikizingatiwa kuna pengo la pointi moja inayowatenganisha na Taifa Stars kwenye msimamo wa kundi lao?
Mamadou: Ushindi wa Tanzania umetengeneza sana vichwa vya habari vya magazeti. Pia nadhani ushindi huu umeiletea heshima kubwa nchi yenu kwenye soka, ni mafanikio makubwa.
Ni lini ilikuwa mara ya mwisho kwa Ivory Coast kucheza mechi ya mashindano ya ukubwa kama wa mashindano haya bila uwepo wa nahodha aliyeachwa Didier Drogba?
Mamadou: Hii sio mara ya kwanza kwa drogba kutokuwemo kwenye kikosi cha Cote, nakumbuka hata kwenye mechi za kuwania kufuzu kwenye AFCON 2012 Drogba hakucheza mechi nyingi, pia kwenye AFCON 2013 kuna alianzia benchi. Timu yetu ya Taifa haina upungufu kwenye ushambuliaji, Drogba kwa sasa hana umuhimu mkubwa, na kwa upande wangu nadhani hakustahili hata kuwemo kwenye kikosi kilichoshiriki AFCON 2013.
Hatimaye uchaguzi wa CAF hivi karibuni umemrudisha tena Issa Hayatou madarakani kwa kipindi kingine. Je ni yapi maoni yako kuhusu ushindi wake?

![]() |
| Kamati kuu ya CAF. |
Mamadou: Nadhani hii
ni aibu kubwa kwa soka la Afrika, kwa kitendo cha Issa Hayatou
kuwarubini maraisi wa vyama vya soka barani Afrika kuwafanya marekebisho
ya sheria ya uchaguzi ili kuweza kumuondoa kwenye kugombea nafasi ya uraisi bwana Shaka. Hii inanikumbusha miaka ile ya nchi za
Afrika kufanya uchaguzi kwa kuchagua mtu mmoja kupitia mfumo wa sera ya
chama kimoja. Hili suala linarudisha nyuma maendeleo ya mpira ndani ya
bara letu. La kusikitisha zaidi kuhusu wafanya maamuzi wa CAF, ni kwamba
Amadou Diakite wa Mali ambaye alifungiwa na FIFA kwa tuhuma za rushwa
michezoni anaruhusiwa kuingia kwenye kamati kuu ya CAF ambayo inatoa
maamuzi ya kumpitisha Hayatou agombee pekee yake. Pia Anjorin Musharraf ambaye alifungwa nchini kwake kwa kugundulika kujihusisha na rushwa michezoni pamoja na kula fedha za udhamini michezoni, na baada ya kutoka kwa dhamana,
Issa Hayatou akamruhusu kuingia kwenye kamati ya kuu ya CAF. Hili
linakupa picha kwamba CAF ni nyumba inayonuka rushwa chafu yenye sumu ambayo imeanza kusambaa kwenye vyama vya soka vya nchi wanachama, ambao
baadhi yao wameonekana kuanza kuiga njia ya Hayatou kwa kubadili katiba
au sheria za uchaguzi kwa manufaa yao. Na pindi baadhi ya watu au
serikali inapoingilia utaratibu huo mbovu, viongozi wa shirikisho wanakimbilia FIFA kusema vyama vinaingilia na mamalaka nyingine za nchi ili FIFA watishie kuifungia nchi na hatimaye serikali ziogope na viongozi wa mashirikisho waweze kutimiza azma zao. Kamati kuu yote ya CAF imejaa wala rushwa na viongozi wabinafsi wenye kuangalia
maslahi yao binafsi. Hayatou na wenzie wote ni wamoja. Raisi wa sasa wa
shirikisho la soka la Tanzania ni mjumbe wa kamati kuu, yeye ni mmoja
ya wafuasi wa Hayatou. Kama sio kama anaona upuuzi wote unaofanyika chini ya kamati yao ilibidi awajibike kujitoa kwa kujiudhuru kwenye kamati hiyo, lakini hakuna anayefanya hivyo. Wajumbe wote wa kamati kuu ni wamoja na wanasapoti vyote anavyofanya Issa Hayatou."
KWA HISANI KUBWA YA SHAFFIH DAUDA in Sports

Post a Comment