MAMLAKA ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeshauri wananchi kutokupiga
au kupokea simu zao za mkononi mvua inaponyesha, hasa ile yenye radi
huku wakiwa nje ya nyumba zao, badala yake wafanye hivyo wakiwa ndani.
Meneja wa Mipango na Utafiti wa TCRA, Dk. Ali Simba, alisema hayo
alipoulizwa swali na waandishi wa habari kuhusu athari zinazotokea kwa
wananchi wanaotumia simu za mkononi ambao wanaishi maeneo yenye mvua za
radi.
Alisema si kwa simu za mkononi tu, hata kwa simu za waya nazo zina athari kubwa zaidi.
“Kunapokuwa na mvua ukawa nje, unashauriwa usitumie simu ya mkononi. Ukiwa ndani simu haina tatizo,” alisema.
Pia alizungumzia suala la simu na athari za maeneo ya uzazi kuwa
hazisababishi watu washindwe kupata watoto au kupunguza nguvu za kiume.
Alisema tafiti mbalimbali zimefanyika lakini hazijaweza kuthibitisha
kama mionzi ya simu za mkononi zinapunguza nguvu za kiume.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Profesa John Nkoma,
alisema mara zote TCRA imekuwa ikiwashauri watu wanunue simu zenye
viwango.
“Ni suala gumu lakini ushauri ni kununua simu zenye viwango. Hapa
Tanzania watu hawana uwezo wa kununua vitu vya gharama kubwa,” alisema
Nkoma.
Pia aliwaondoa hofu Watanzania kuwa mionzi inayotumika kwenye vyombo vya mawasiliano haina madhara ya aina yoyote.
NA TANZANIA DAIMA
Post a Comment