Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

RAGE AWAKASHIFU SIMBA

MWENYEKITI wa Simba SC, Ismael Aden Rage, amesema mapinduzi yaliyofanywa na wanachama wa klabu hiyo, ni kinyume cha Katiba na hayawezi kumng’oa madarakani. Rage ametoa kauli hiyo juzi, wakati akizungumza katika kipindi cha Sports, kinachorushwa na Radio One, ambapo amesema mkutano huo ni batili na bado yeye ni Mwenyekiti halali wa Simba.
“Mapinduzi hayo ni batili na ni kinyume cha Katiba ya Simba, kwanza siku hizi mambo ya kupinduana hakuna, sasa kama wao wamefanya mapinduzi waende klabu.

“Mkutano huo waliofanya ni kikao cha harusi, wala hawawezi kuning’oa madarakani, wasubiri mimi nirudi ndio tufanye mkutano wa wanachama, mimi nipo India kwa matibabu na siwezi kutoka hadi daktari wangu aniruhusu,” alisema Rage.

Wakati Rage akisema hayo, tayari uongozi wa klabu hiyo umepeleka barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutotambua mkutano huo, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Starlight, jijini Dar es Salaam.

Kwa sasa klabu ya Simba hali si shwari, tangu kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zakaria Hans Poppe na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange Kaburu, huku wanachama wakitaka Rage naye aachie madaraka kutokana na mwenendo wa timu yao kufanya vibaya.

NA MTANZANIA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top