WANANCHI wa Kenya leo wanapiga kura kuwachagua viongozi wao
katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza baada ya kupata Katiba Mpya, ambao
unawapambanisha vikali watoto wa waasisi wa taifa hilo ambao sasa ni
marehemu.
Uchaguzi wa leo unaelezwa kuwa na kinyang’anyiro
kikali ambacho hakijawahi kushuhudiwa baina ya wagombea wawili wa urais,
Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee na Raila Odinga wa Cord.
Uhuru ni mtoto wa Rais wa kwanza wa Kenya, Mzee
Jomo Kenyatta wakati Raila ni mtoto wa aliyekuwa makamu wa Kenyatta,
Jaramog Oginga Odinga.
Mbali na wagombea hao wenye matumaini ya kuingia
Ikulu kila mmoja, wapo wengine sita – Musalia Mudavadi (UDF), Peter
Kenneth (Eagle Alliance), Martha Karua (Narc), Mohammed Abduba Dida
(ARK), Prof James ole Kiyiapi (RBK) na Paul Muite wa Safina.
Wagombea wote walihitimisha kampeni zao Jumamosi
na jana hakukuwa na kampeni kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi ya Kenya.
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC), imesema maandalizi yote
yamekamilika na vifaa vyote vya kupigia kura vimeshafika katika maeneo
husika.
Mwenyekiti wa IEBC, Ahmed Hassan alisema katika
taarifa yake jana kuwa vituo vitafunguliwa saa 12:00 asubuhi na kufungwa
saa 1:00 jioni, lakini kama kutakuwa na wapigakura kwenye foleni
wataendelea hadi watakapokuwa wamemaliza kupiga kura.
Kwa mujibu wa Hassan, kura zote zitahesabiwa vituoni na matokeo kutumwa kwa njia ya simu>>>>>>>>>>>>>HABARI KAMILI ENDELEA HAPA
Post a Comment