Vijana machacahari Mtela Mwampamba na Juliana Shonza walioihama Chadema 
hivi karibubi, wakiserebuka nje ya Ofisi ya CCM mkoa wa Morogoro, baada 
ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa, 
 Sadifa Hamis Juma kuwasili kwenye ofisi hiyo, Februari 28, 2013 kuanza 
ziara ya siku tatu mkoani humo.
Sadifa akipatiwa burudani ya shairi na mmoja wa waghani maarufu wa 
mashairi mkoani Morogoro.Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus
 Mapunda
Mwenyekiti wa UVCCM, Sadifa Hamis Juma akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa 
Morogoro, Sixtus Mapunda wakati wa mkutano wa ndani kati ya Mwenyekiti 
huyo na wajumbe wa Baraza la Vijana mkoa wa Morogoro
Mkuu wa Utawala wa UVCCM Taifa, Abdallah Mpokwa akitoa utambulisho wa 
watu walioambatana na Sadifa kwenye msafara huo, katika ukumbi wa CCM 
mkoa wa Morogoro
Kada wa CCM aliyehamia kutoka Chadema hivi karibuni, Mtela Mwampamba akisalimia baada ya kutambulishwa ukumbini.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, Juma Borafya 
akisalimia baada ya kutambulishwa kwenye kikao hicho cha ndani. Wapili 
kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro mjini, Ali Issa, Naibu Katibu 
Mkuu wa UVCCM, Taifa, Mfaume Kizigo na Sixtus Mapunda
VIVA VIJANA VIVAAAA!!!!!, Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Sixtus Mapunda 
akiongoza salaam maalum kwa Vijana wa UVCCM ukumbini. Pamoja naye kutoka
 kulia ni Katibu wa CCM Morogoro, Ali Issa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM
 Mfaume Kizigo. Walioketi kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro 
Harrieth Sutta na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa.
VIVAAAA!!!, vijana wakiitikia salam ya Sixtus ukumbini, baadhi yao ni Shonza na Abubakar Assenga
VIVAAAA, VIVAAAA!!!!, Vijana wakiitikia  salam
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Morogoro Herieth Sutta akimkaribisha Sadifa kuzungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Sixtrus Mapunda
 NAFURAHI KUWA NA WEWE! Sadifa akimwambia Sixtus Mapunda kabla ya kuanza
 hotuba yake ya mkutano huo wa ndani uliofanyika Ofisi ya CCM mkoa wa 
Morogoro
Sadifa akizungumza kwenye mkutano huo wa ndani
Sadifa akisisitiza jambo
Na kusisitiza zaidi
Sadifa akizidi kusisitiza hotuba yake huku viongozi wakiwa makini kumzikiliza
ULIOCHAGULIWA MSIJIKWEZE, JISHUSHENI KWA WANACHAMA", Anasema Sadifa
 "Wapendeni waliowapinga wakati wa uchaguzi" msiwanunie, kama mtu 
hakukuunga mkono leo kwa hili ipo siku atakuunga kwa jengine", akasema
Sadifa akitoka na wenyeji wake ukumbini 
(Picha na CCM Blog) 

















Post a Comment