Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia
.................
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia, na kufafanua kuwa maazimio hayo yametokana na kikao kilichofanyika juzi kati ya viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge bungeni , Spika wa Bunge, Anne Makinda, watendaji wake pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi.
Mbatia alisema wameshuhudia katika vikao vya Bunge baadhi ya wabunge kushabikia zaidi vyama vyao badala ya kujadili masuala muhimu yenye maslahi kwa umma.
“Unakuta chama kinakuwa na ushabiki ndani ya Bunge kikibishania maslahi ya chama chake badala ya kuzungumzia mambo yenye maslahi kwa wananchi na taifa,” alisema Mbatia na kuongeza:
“Wabunge wengine wana nidhamu ya uoga hata pale zinapowasilishwa hoja za msingi ambazo ni za maslahi ya taifa, wabunge wa vyama vingine wanakataa kuunga mkono kwa mfano, hoja ya ajira aliyoiwasilisha Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, hoja ya maji ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na hoja ya elimu niliyowakilisha mimi, hakuna mbunge wa Chama cha Mapinduzi aliyeunga mkono. Hii inaonyesha jinsi bunge linavyoshindwa kufanya kazi yake.”
“Tunatakiwa tuweke itikadi za vyama pembeni katika masuala muhimu yenye maslahi ya taifa. vyama visambaratike, lakini taifa kwanza,” alisema.
Aidha baadhi ya maazimio mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni pamoja na vyama kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wabunge kwenye mafunzo mbalimbali, ili ili waweze kutekeleza majukumu yao ndani na nje ya Bunge, taifa, majimbo yao na vyama vyao.
CHANZO:
NIPASHE
Post a Comment