Kikosi cha timu ya Young Africans Sports Club mara baada ya mazoezi
ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini kijitonyama, kimeingia kambini
katika hosteli za klabu zilizopo makao makuu ya Yanga mitaa ya
Twiga/Jangwani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya timu ya
Toto Africans siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.
Wachezaji wote wameingia kambini kwa ajili ya kujianda
ana mchezo huo wa jumamosi ambao Yanga inahitaji kupata pointi 3 muhimu
ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kuongoza
msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom na hatimaye kutwaa Ubingwa.
Katika
mazoezi ya leo wachezaji watatu (3) hawakuweza kufanya mazoezi kutokana
na kuwa matatizo tofauti, wachezaji hao ni Ally Mustafa 'Barthez'
(tumbo), Juma Abdul (malaria) na Nurdin Bakari (goti), daktari wa timu
Dr Nassoro Matuzya amesema wachezaji hao wanaendelea vizuri na huenda
kesho wakajumuika na wachezaji wengine katika mazoezi ya asubuhi.
Baada
ya kuichapa timu ya Kagera Sugar kwa bao 1-0 katika mchezo uliopita
mwishoni wa wiki, timu ya Young Africans Sports Club itashuka dimbani
siku ya jumamosi kucheza na timu ya Toto Africans ya kutoka jijini
Mwanza, mchezo utakaofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar
es salaam kuanzia majira ya saa 10 jioni.
Young
Africans ambayo inaongoza msimamo wa ligi kuu ya VPL itashuka dimbani
kusaka pointi 3 muhimu ambazo zitaendelea kuifanya iendelee kuongoza
msimamo wa ligi kuu lakini pia kushinda mchezo huo itakua ni kuendeleza
ushindi mfululizo ktika michezo yake ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara.
Katika mchezo wa mzunguko
wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Toto African dhidi ya Yanga
mchezo uliofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, watoto wa
Jangwnai Yanga waliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-1, mabao
yaliyofungwa na Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na Mbuyu Twite.
Young
Africans yenye jumla ya point 42 na mabao 35 ya kufunga na mabao 12 ya
kufungwa itashuka dimba la uwanja wa Taifa kuhakikisha inaibuka na
ushindi katika mchezo huo dhidi ya timu ya Toto African ambayo inakamata
nafasi ya pilli kutoka mwisho katika msimo wa ligi kuu ya Vodacom
nchini kwa kuwa na point 14.
Post a Comment