CHAMA cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo Mikoani (TABOA), kimesema msimamo
wake wa kutumia nauli mpya ambazo zinatarajia kuanza kutumika rasmi
Ijumaa ya wiki hii, uko pale pale.
Akitoa tamko la chama hicho kwa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa TABOA, Ennea Mrutu alisema msimamo wao uko pale pale kutokana na ukweli kuwa wamiliki wa mabasi wanatumia gharama kubwa kuhudumia wananchi.
“Nawaomba Watanzania watuelewe, hatuna nia mbaya katika hili, tunasisitiza kwamba nauli mpya zilizotangazwa, zitaanza kutumika Ijumaa ya wiki hii, hakuna mabadiliko katika hili.
“Wamiliki tumekuwa tukitumia gharama kubwa mno kuendesha mabasi haya…tunabanwa na mambo mengi yakiwamo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), vipuri vya magari, mafuta na mishahara ya wafanyakazi,” alisema Mrutu.
Akitoa mfano alisema, wamekuwa wakiingiza mabasi mapya nchini kwa gharama kubwa, lakini siku zote Serikali imeshindwa kuwaondolea VAT, jambo ambalo wanaona ni kama ukandamizaji kwao.
Mbali ya kilio hicho, Mrutu alisema hivi sasa wanalazimika kulipa gharama kubwa ya ushuru katika halmashauri nyingi, jambo ambalo limekuwa likiwakwaza wamiliki.
“Tunatumia gharama kubwa kulipa ushuru kwenye halmashauri za wilaya, sasa tusipopandisha nauli sisi tutawezaje kuendesha vyombo hivi? Alihoji Mrutu.
Kuhusu malalamiko yanayotolewa na Chama cha Kutetea Haki za Wasafiri (CHAKUWA), kuwa hawakushirikishwa wakati wa mchakato wa kupandisha nauli, Mrutu alisisitiza madai hayo hayana msingi wowote.
“Tangu tunaanza mchakato huu, tulishirikisha wadau wote wakiwamo hao CHAKUWA, sasa sijui malalamiko haya yasiyokuwa na tija yanatoka wapi, tunasema msimamo wetu wa nauli upo pale pale, tunaomba watuunge mkono katika hili, sisi tunasubiri nauli hizi kwa hamu sana,” alisema Mrutu.
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa TABOA, Severine Ngallo aliwataka Watanzania watambue kuwa wamiliki wa mabasi wanatoa huduma hivyo wanapaswa kuungwa mkono.
“Sisi tunafanya kazi ya kuhudumia Watanzania, wana kila sababu ya kutuunga mkono katika hili na tunawahakikishia watapata huduma nzuri tu,” alisema Ngallo.
Kuhusu madai ya CHAKUWA, alisema wamiliki wa mabasi wanahisi chama hicho kinatumiwa na wanasiasa kwa manufaa yao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TABOA Mkoa wa Dar es Salaam, Hamza Mringo aliitaka Serikali kuweka utaratibu wa kuwapa wamiliki fidia pindi wanapopakia wanafunzi kama ilivyo katika nchi za Ulaya.
“Tunapakia wanafunzi wanalipa nauli nusu, lakini hatulipwi fidia, tunadhani umefika wakati tuanze kulipwa kila mwisho wa mwezi ili kupunguza gharama zinazotukabili,” alisema Mringo.

NA MTANZANIA
Post a Comment