Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Mwenyekiti wa Makampuni
ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia shilingi milioni 100 kwa
ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha
Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika Jumamosi usiku katika
hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba akimshukuru
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia
shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo
Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye hafla ya harambee iliyofanyika
Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi,
Mufti wa Tanzania Sheikh Issa bin Shaaban Simba, KATIBU Mkuu wa Baraza
la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Suleman Lolila (wa pili
kulia), Kadhi Mkuu Sheikh Abdallah Mnyasi (kulia) na Shehe wa Mkoa wa
Dar es salaam Alhaj Alhad (kushoto) wakiomba dua baada ya harambee
kusaidia upanuzi na maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain
kwenye hafla iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini
Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi ambaye alichangia
shilingi milioni 100 na Mwenykiti wa NCCR-Mageuzi Mhe James Mbatia
aliyechangia shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia upanuzi na
maendeleo ya Chuo Cha Kiislamu cha Al-Haramain kwenye harambee
iliyofanyika Jumamosi usiku katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Rais Kikwete akihutubia kwenye harambee ya kuchangia upanuzi wa ujenzi Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Al- Haramain
(Chanzo: Ikulu).
Post a Comment