Kwa ufupi
Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya
Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini)
na Ezekiah Wenje (Nyamagana).
,,,,,,,,,,,,,,
,,,,,,,,,,,,,,
Wakitangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi ya Mbugani, Mwanza jana, walisema pia watakwenda kwenye majimbo ya wabunge wawili wa CCM, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera) ili kueleza jinsi wabunge wa upinzani wanavyokandamizwa bungeni.
Ndugai, ambaye ni Mbunge wa Kongwa (CCM),
aliwasimamisha wabunge sita wa Chadema kuhudhuria vikao vitano vya Bunge
kutokana na kile alichokiita kufanya vurugu bungeni. Hatua hiyo ya
Ndugai aliyoichukua Aprili 17, mwaka huu ilipata baraka za Spika Makinda
Ijumaa iliyopita.
Wabunge waliosimamishwa ni Tundu Lissu (Singida
Mashariki), Godbless Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya
Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini)
na Ezekiah Wenje (Nyamagana). Katika mkutano huo ulioanza saa 9.30
alasiri na kumalizika saa 12.00 jioni, ulihudhuriwa na wabunge wanne
kati ya hao. Mbilinyi ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhutubia akifuatiwa
Mchungaji Msigwa, Kiwia na Wenje. Lissu na Lema hawakuhudhuria.
Akizungumzia ziara yao katika majimbo ya viongozi
hao wa Bunge, Mchungaji Msigwa alisema itakuwa ya kuwashtaki kwa
kuendesha Bunge kuwapendelea wabunge wa CCM hata wanapofanya makosa ya
wazi.
Alidai kuwa wabunge wa CCM ndiyo vinara wa lugha
chafu bungeni na kuwatolea mfano Mwigulu na Lusinde. Pia alizungumzia
tusi zito lililotolewa na Mbunge wa Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba,
Aprili 17, mwaka huu.
“Kila mtu alimshuhudia Serukamba alipoporomosha tusi zito, lakini Spika na Naibu wake hawakuchukua hatua zozote.
“Kila mtu alimshuhudia Serukamba alipoporomosha tusi zito, lakini Spika na Naibu wake hawakuchukua hatua zozote.
“Lissu na sisi wengine tumeadhibiwa kwa kosa la
kuomba mwongozo wa Spika. Hapa wananchi mnaona kuna haki kweli,?”
alihoji Mchungaji Msigwa huku akishangiliwa na wafuasi wa chama hicho.
Alisema watapita kwenye majimbo ya wabunge wa chama hicho waliosimamishwa ili kuwaelimisha wapigakura wao.
Alisema wataanza ziara majimboni kesho wakianzia
Iramba Magharibi kumshtaki Nchemba. Baada ya hapo watakwenda Singida
Mashariki kwa Lissu ili kuwapa ukweli wapigakura wake.
Mchungaji Msigwa alisema baada ya hapo watakwenda Kongwa kwa Ndugai na kisha Mtera kwa Lusinde kabla ya kuelekea Njombe Kusini kwa Makinda. Pia watakwenda Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha.
Mchungaji Msigwa alisema baada ya hapo watakwenda Kongwa kwa Ndugai na kisha Mtera kwa Lusinde kabla ya kuelekea Njombe Kusini kwa Makinda. Pia watakwenda Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha.
Hata hivyo, ziara ya wabunge hao kwenda mkoani
Mbeya imekwaa kisiki baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya,
Athumani Diwani kukataa kutoa kibali.
Kumlipua kigogo CCM
Mchungaji Msigwa ameahidi pia kulipua bomu la kigogo wa ngazi ya juu wa CCM, ambaye alidai kuwa anajihusisha na ujangili wa meno ya tembo atakaporejea bungeni baada ya kumaliza adhabu yake wiki hii.
Mchungaji Msigwa ameahidi pia kulipua bomu la kigogo wa ngazi ya juu wa CCM, ambaye alidai kuwa anajihusisha na ujangili wa meno ya tembo atakaporejea bungeni baada ya kumaliza adhabu yake wiki hii.
Wenje ataja safu ya 2015
Wenje aliwaambia wafuasi wa chama chake kuwa kimejipanga kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2015 na CCM wanapaswa kujipanga kuondoka madarakani.
Wenje aliwaambia wafuasi wa chama chake kuwa kimejipanga kushinda Uchaguzi Mkuu wa 2015 na CCM wanapaswa kujipanga kuondoka madarakani.
Alitoa kali alimpotaja Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Willbroad Slaa kuwa Rais na Freeman Mbowe, Waziri Mkuu. Wengine
aliowataja na kuwapa vyeo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
(Waziri wa Fedha), Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Kilimo), Lema (Mambo ya
Ndani), John Mnyika (Nishati) na Wenje (Mambo ya Nje).
NA MWANANCHI
NA MWANANCHI
Post a Comment