Kikosi cha timu ya Young Africans Sports Club leo kimeanza tena
mazoezi baada ya kuwa na mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu ya
Pasaka katika uwanja wa mabatini Kijitonyama, kujiandaa na mchezo
unaofuata dhidi ya timu ya JKT Oljoro kutoka jijini Arusha mchezo
utakaofanyika Aprili 10 2013.
Young Africans ambayo mwishoni mwa wiki ilitoka suluhu ya bila
kufungana na timu ya Polisi Morogoro, bado inaendelea kuongoza msimamo
wa Ligi Kuu kwa kuwa na poniti 49, zikiwa ni pinti sita (6) mbele ya
timu ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 43.
Katika
mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Jamhuri mjiji Morogoro, ulikosa
radha kutokana na waamuzi kutokua makini na kutofautiana katika maaamuzi
mbali mbali hali iliyopelekea mchezo kuishia kwa sare ya tasa 0-0.
Baada
ya suluhu ya jumamosi kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi leo asubuhi
kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya timu ya JKT Oljoro ambayo katika
mchezo wa awali uliofanyika jijini Arusha, watoto wa jangwani waliibuka
na ushindi wa bao 1-0, bao lililofungwa na mlinzi Mbuyu Twitew.
Yanga
imebakisha jumla ya michezo mitano (5) ili kukamilisha michezo ya
mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom 2012/2013, michezo iliyobaki ni
kama ifuatavyo:
Aprili 10, 2013 : Young Africans Vs JKT Oljoro (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
Aprili 13, 2013 : Mgambo Shooting Vs Young Africans (Mkwakwani - Tanga)
Aprili 21, 2013 : JKT Ruvu Stars Vs Young Africans (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
May 01, 2013 : Young Africans Vs Coastal Union (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
May 18, 2013 : Simba SC Vs Young Africans (Uwanja wa Taifa - Dar es salaam)
Wachezaji waliofanya mazoezi leo ni :
Walinda mlango: Ally Mustafa 'Barthez' na Yusuph Abdul
Walinzi: Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Oscar Joshua, Juma Abdul, Godfrey Taita, Kelvin Yondani na Nadir Haroub 'Cannavaro'
Viungo: Omega Seme, Salum Telela, Nurdin Bakari, Frank Domayo, Rehani Kibingu, David Luhende na Haruna Niyonzima
Washambuliaji: Said Bahanuzi, Saimon Msuva, Hamis Kiiza, George Banda, Nizar Khalfani na Didier Kavumbagu
Wachezaji
ambao hawakuweza kushiriki katika mazoezi ya leo ni mlinda mlango Said
Mohamed na Jerson Tegete ni majeruhi, Athuman Idd 'Chuji' anayeumwa
tonses na mlinzi Mbuyu Twite ambaye anauguliwa na mkewe.
Post a Comment