Gadna G Habash |
AKIONGEA NA MTANGAZAJI DAN CHIBO MTANGAZAJI WA TBC FM,NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA
Leo
nilipata nafasi ya kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na
Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya
maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?
Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo
anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu
naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi
nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara
nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au
kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu
mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya
Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema lakini
siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona
hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa
kisabuni.
Hii ni kama vita mmejipangaje..?
Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa
halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama
watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu
wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu
kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma
sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona
kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo
Nini mlikiona kama chokochoko...?
Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina,
ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado
alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda
sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona
umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye
grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa
ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.
Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?
Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni
ya redio inategamea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla kwa
kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata
hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila
tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari
fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu
wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani
lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa
madhara nisiposema.
Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?
Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine
unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui
wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako
unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza
kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa.
Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana
jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa,lakini wakati
wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi
inatosha....
Kauli yako ya mwisho ni ipi..?
Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu
yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea
kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli
na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee
kukosea wabadilikee….
Mwisho..!
1 comments:
Post a Comment