Msajili wa Vyama vya siasa nchini, John Tendwa
,,,,,,,,,,,,,,,,
Dar es Salaam. Ikiwa imebaki miezi miwili
Tanzania itimize miaka 21 tangu iingie katika mfumo wa vyama vingi vya
siasa, Msajili wa Vyama vya siasa nchini, John Tendwa amesema hoja
nyingine zinazotolewa na vyama vya upinzani ni za msingi na zinatakiwa
kufanyiwa kazi.
Amesema katika kipindi cha miaka 21, vyama vya
upinzani vimeimarika na viongozi wake wametoa hoja za msingi kwa
maendeleo ya taifa, huku akisisitiza kuwa kama vikisema ukweli unatakiwa
kufanyiwa kazi na siyo kubezwa.
Mfumo wa chama kimoja ulidumu kwa miaka 27
(1961-1992), ulibadilishwa ili kuurejesha mfumo wa vyama vingi vya siasa
kutokana na marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
sheria namba 5 ya mwaka 1992.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana,
Tendwa alisema demokrasia imekuwa kwa kiwango kikubwa na kutolea mfano
mvutano kati ya CCM na Chadema, akisema kuwa unatakiwa kuchukuliwa kama
mgongano wa kisiasa na si vinginevyo.
“Kikubwa ambacho viongozi wa chama tawala na wale
wa upinzani wanatakiwa kujihadhari nacho ni lugha za matusi na
kujihusisha na mambo ambayo yanaweza kuleta uvunjifu wa amani,” alisema
Tendwa na kuongeza;
“Pamoja na mivutano iliyopo ukweli unabaki palepale kwamba vyama vipo vingi na vyote haviwezi kuibuka na ushindi.”
“Pamoja na mivutano iliyopo ukweli unabaki palepale kwamba vyama vipo vingi na vyote haviwezi kuibuka na ushindi.”
Alisema hata nchini Marekani, Chama cha Republican
na Democratic vina upinzani mkali na wakati mwingine viongozi wake
hurushiana maneno ya hapa na pale, “hiyo ndiyo siasa ya vyama vingi.”
Alisema asilimia 80 ya kazi ya siasa ni propaganda
na alisisitiza kuwa yanayozungumzwa na wapinzani yanalenga kuwaeleza
Watanzania kuwa CCM haijafanya lolote.
NA MWANANCHI
NA MWANANCHI
Post a Comment