Meya
wa Jiji la Arusha, Ndugu Gaudence Lyimo akihutubia wakazi wa kata ya
Themi na kuwataka wasifanye makosa katika uchaguzi huu.
Rehema
Mohamed maarufu kama Iron Lady akihutubia wakazi wa kata ya Themi
ambapo aliwataka wakazi hao kuwa makini sana na wanasiasa wasiokuwa na
mipango ya maendeleo.
Kikundi
cha ngoma cha Kambarage kikiburudisha wakazi wa kata ya Themi wakati wa
mkutano wa kampeni za udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
Kijana
anayefahamika kwa jina la Mboya ambaye alikuwa mstari wa mbele katika
harakati za Chadema,akihutubia wakazi wa kata ya Themi wilaya ya Arusha
mjini na kuwaambia wasirudie kuchagua vyama ambavyo kura yao itapotea
kwa matapeli wa kimataifa.
Nico
ambaye naye alikuwa mstari wa mbele kuongoza mipango michafu ya
kuvuruga amani ya Arusha, amekiri kuwa chama pekee cha kisiasa Tanzania
kwa sasa ni CCM na ameomba wakazi wa kata ya Themi kuungana na kumchagua
diwani anayetokana na CCM ili kuleta maendeleo na si migomo.
MNEC
wa wilaya ya Arusha mjini Godfrey Mwalusamba akihutubia wakazi wa kata
ya Themi,ambapo aliwaambia kuna uhumu wa kufanyia kazi maendeleo yao
zaidi kuliko kushabikia vitu visivyo na tija.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Themi
na kuwaambia wasirudie kosa la kudharauliwa kwa kuchagua watu
wasiotambua thamani ya kura zao.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahakikishia wana Themi kuwa
wakati huu ni wa kuirudisha heshima ya Arusha na kwa kumchagua mgombea
wa CCM kutasaidia sana kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika mji huo.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa kiti cha
udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe, Juni, 13,2013 .
Mgombea
wa kiti cha udiwani kata ya Themi, Victor G. Mkolwe akihutubia wakazi
wa kata hiyo na kuwaelezea moja ya mikakati yake ya kuleta maendeleo kwa
wakazi hao,ambpo pia aliwaambia yeye hatangulizi siasa bali maendeleo
na anatambua wakazi wake vizuri na changamoto zao na namna ya
kuwasaidia.
Mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Arusha, Catherine Magige akihutubia wakazi wa
kata ya Themi ambapo pamoja na kuwaomba kumpigia kura mgombea wa udiwani
kwa tiketi ya CCM pia aliahidi kuwasaidia wakina mama Wajane ambao
walitelekezwa na ahadi za uongo za vyama upinzani.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na baadhi ya wakina
mama Wajane ambao walidanganywa na vyama vya upinzani na sasa wamerejea
CCM.
Wajane wa kata ya Themi wakisalimiana na mbunge wa viti maalum wa mkoa wa Arusha ,Catherine Magige.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na vijana wa Arusha
mjini waliokuwa wakijiburudisha na mchezo wa karata.














Post a Comment