Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

TASWIRA:KILICHOJIRI KESI YA MAKADA WA CHADEMA TABORA

Jana nikiwa mahakamani Tabora kulia kwangu ni M/Kiti wa Chadema Tabora Kamanda Mbaruk, kushoto ni shemeji yangu Kamanda Bella.

Jana ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia MAHAKAMA KUU ambapo nilishuhudia jaji akifanya kazi yake kwa busara iliyopitiliza (kwa maoni ya Wakili msomi Peter Kibatala) 

Kamanda wangu Mume wangu (kombati nyeusi) na shemeji zangu wakiingia mahakamani jana mjini Tabota. 

Masuala ya Mahakamani yanaitaji subira ya hali ya juu hivyo bado naendelea kumfariji Mpenzi wangu Kilewo ya kwamba mambo haya yatapita tu. zaidi ya hapo namwombea sana.
Kushoto kwangu ni kamanda wa Chadema Tabora (huyu mama) na kulia ni mke mwenzangu (mumewe yupo kesi moja na mume wangu)

Kwa maoni ya Wakili Msomi PK ni kwamba Jaji alichukulia kesi hiyo kwa uzito wake na pia akaheshimu na kuzingatia hali halisi ya Wakili, kwamba anatoka mbali Dar es salaam na hivyo akaamuru Hoja za pande zote mbili zipelekwe kimaandishi kuwaondolea usumbufu hasa wapeleka maombi ambao ni sisi tunaosafiri kila siku. Na kwa sababu hizo basi tar 30july Jaji atataja tar ya uamuzi. 

Asanteni sana sana najua mpo pamoja na familia yetu.
CHANZO:Talk Show.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top