Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasilimia baadhi ya viongozi
wa CCM, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege mjini Mtwara asubuhi
hii, tayari kwa safari ya kwenda katika mikoa ya Ruvuma na Mbeya kuanza
ziara yake ya siku 22 katika mikoa hiyo kesho. Kabla ya kuwasili katika
mikoa hiyo, akiwa mkoani Mtwara leo atakutana na Wajumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM wilayya Masasi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, wakisalimiana na viongozi
wa CCM baada ya kuwasili na Kinana mjini Mtwara asubuhi hii.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Mkuu wa mkoa wa
Mtwara, Kanali Joseph Simbakalia, Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Kinana akiwa na viongozi wa mkoa wa Mtwara