Nyumba
ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea ikiwa
inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi
kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua kuichoma
moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi.
Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali
Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
Segerea,
Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea
Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba
hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.
Hali
hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa
Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo
inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya
kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje
na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia
moto nyumba hiyo.
Mmoja
wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu
Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa
mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto
wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke
anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo
Mpaka
Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea
kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili
ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba
hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au
laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo
zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto
kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile
za kuuzima mot huo.
Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.
CHANZO:Josephat Lukaza - Lukaza Blog, Dar Es Salaam.