Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akimkabidhi mbele ya wananchi
mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Boneventura Kiswaga, Ilani ya uchaguzi
ya 2015/2020 atakayoisimamia katika kuwaletea maendeleo wananchi wa
jimboni humo.Picha Na Peter Fabian.
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu.
Katibu
wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, akimkabidhi mbele ya wananchi
mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Boneventura Kiswaga, Ilani ya uchaguzi
ya 2015/2020 atakayoisimamia katika kuwaletea maendeleo wananchi wa
jimboni humo.
Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, Bonevetruta Kiswaga akiwaomba
wananchi wamchague kuwa mwakilishi wao katika Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania jana katika Uwanja wa mpira Magu mjini waliofurika
kumsikiliza akinadi sera zake.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Bonevetura Kiswaga.
NA PETER FABIAN,MAGU.
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza kimeomba radhi kwa wananchi wa Jimbo
la Magu mkoani humo kukichagua ili kumaliza kabisa kero na matatizo ya
maji safi katika Mji wa Magu na maeneo yanayokabiliwa na changamoto
hiyo.
Akihutubia mamia ya wananchi
waliofurika katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge na Udiwani
jimboni humo jana uliofanyika katika uwanja wa mpira wa mjini Magu,
Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu, alisema kwamba tatizo hilo
linashughulikiwa na serikali na liko katika hatua nzuri ya kupunguza
maumivu ya uhaba wa maji safi.
Mtaturu
aliwaeleza wananchi kwamba kumekuwa na kero ya muda murefu ya upungufu
wa maji safi na kusababisha kuwepo changamoto kubwa ya kuhangaika kupata
huduma ya maji safi katika mitaa, vitongoji na vijiji vya mji wa magu.
“Tumeikumbusha
serikali kwa mara kadhaa na kukubali kuweka bajeti ya kujenga mradi
mkubwa wa maji safi kutoka Ziwa Victoria ambao utaweza kuhudumia Mji huu
na maeneo mengine ambao utanaraji kuanza kujengwa mwishoni mwa mwaka
huu baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na kutangwazwa kwa zabuni
ili kumpata Mkandarasi,”alisema.
Katibu
huyo aliwaomba wananchi kuwachagua Bonaventura Kiswaga kuwa Mbunge wa
Jimbo hilo kutokana na kufanya kazi zinazoonekana akiwa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya hiyo aliyemaliza muda waka ili aweze kusimamia na
kupigania maendeleo ya jimbo hilo lakini pia kusimamia Ilani ya CCM na
kushughulikia kero hiyo ya maji safi na zingine za kijamii.
“Kuna
mambo mengi yamefanyika kwenye uwakilishi wa Dk Festus Limbu, aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo hili ambaye hakugombea tena na kuviacha sasa tunahitaji
mtu mwenye upeo, umakini na weredi wa kuyapigania na kusimamia ili
kuhakikisha wananchi wanapata ufumbuzi wa haraka ikiwemo kupata huduma
za kimaendeleo na kiuchumi kupitia sekta zote,”alisema.
Naye
mgombea Ubunge wa Jimbo la Magu, Kiswaga aliwaomba wananchi kumchagua
kuwa mwakilishi wao na kipaumbele chake cha kwanza ni kumaliza kero ya
maji safi na salama katika Miji wa Magu na maeneo ya vitongoji na vijiji
vyenye kukabiliwa na changamoto hiyo pamoja na kuwepo juhudi za
kupunguza makali hayo kutokana na ongezeko la watumiaji huku miundombinu
ikiwa siyo rafiki kwa wakati huu.
Aidha
aliongeza kuwa akiwa mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ameacha mpango
kabambe wa wa kutekeleza mradi wa dhalula wa maji safi ambao utawafanya
wananchi kutotumia kiasi kikubwa cha fedha kupata huduma hiyo na kudai
kuwa utakamilika mwishoni mwa mwezi Novemba wakati serikali kupitia
Wizara chini ya usimamisi wa Mamlaka ya Maji safi na Mazingira ya
Jijijni Mwanza (MWAUWASA) ikiendelea na utaratibu wa kujenga mradi
mkubwa utakaokidhi mahitaji ya wananchi wa mji na vijiji.
Kiswaga
aliwaeleza wananchi waliofurika kumsikiliza endapo watampatia lidhaa ya
kuwa Mbunge wao, alisema kwamba kipaumbele cha pili kitakuwa ni sekta
ya Afya kwa kuhakikisha anasimamia ujenzi wa Vituo ya Afya kila Kata
ikiwemo nyumba za watumishi ili kuwezesha kutoa huduma kwa wananchi kama
inavyokusudiwa na serikali ikiwemo ujenzi wa barabara za changalawe na
lami ikiwemo barabara ya Magu-Ngudu kwa kiwango cha lami.
“Ntahakikisha
suala la Elimu linapata msukumo mkubwa kwa kusimamia ujenzi wa vymba
vya madarasa katika shule za msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na
juenzi wa nyumba za walimu pamoja na kuongeza Sekondari za kidato cha
tano na sita (Haigh School), kukabiliana na changamoto ya upungufu wa
madawati na thamani za maabara tulizojenga kwenye kila sekondari ya
Kata,”alisema.
Kiswaga awaliwaomba wananchi
kumchagua mgombea Urais Dkt John Magufuri, yeye na Madiwani wote
walioteuliwa na CCM kupeperusha bendera ili kuwezesha Ilani ya uchaguzi
ya 2015/2020 inatekelezwa kikamilifu na wananchi wapate huduma
zinazohitajika katika Sekta za Elimu, Afya, Barabara, Kilimo, Mifugo,
Uvuvi, Ajira na Uchumi ili kupiga hatua ya maendeleo
CREDIT: G SENGO
Post a Comment