Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

HOTNEWS.......MAOFISA WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA) WAAMRIWA KUJISALIMISHA POLISI NI BAADA YA UPOTEVU WA MAKONTENA 349 BANDARINI


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa  akiagana na viongozi wa TRA na TPA.

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa  wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.

Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Katika Ziara hiyo ya ghafla Waziri mkuu Kasim Majaliwa awasimamisha kazi kamishna wa kodi Tiagi Masamaki na Habibu Mpozya kitengo cha huduma kwa wateja kutokana ubadhilifu wa fedha kwa makontena zaidi ya 300 yaliyopotea.


Wengine ni Haruni Mpande -ICT, Hamisi Ali Omari na Eliachi Mrema incharge wa ICD na amemuru wrote wakamatwe  uchunguzi uendelee.

Walohamishwa kituo na kupelekwa mikoani ni Nsajigwa Mwandege, Robert Nyoni na  Anangisye  Mtafya

Maofisa hao wametakiwa kusalimisha hati zao za kusafiria hii imekuja baada ya kubainika kuwa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya tsh bilioni 80 hayaonekani katika mtandao wa TRA huku data za mamlaka ya bandari yanataarifa
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top