Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Katibu Mkuu Mambo ya Nje atembelea Makumbusho ya Taifa

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula akiweka saini kwenye kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Jumba la Makumbusho la Taifa lililopo jijini Dar es Salaam. Pembeni yake pichani ni Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw. Achiles Bufure (kushoto) akiwa na mgeni wake. 
Balozi Mulamula (wa tatu kutoka kushoto), akitizama moja ya hati zilizotolewa na  Malkia Elizabeth wakati wa uhuru. Pichani ni Mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dkt. Amandus Kweka (wa kwanza kulia), Bw. Bufure (wa pili kutoka kushoto).
Dkt. Kweka akiendelea kuelezea chimbuko la mwanadamu na Fuvu lililopo kushoto kwenye sanduku lililo nakshiwa na dhahabu ni la Zinjanthropus lililogunduliwa  huko Olduvai Ngorongoro kwenye miaka ya 1959. 
Bw. Bufure akimwonyesha Balozi Mulamula Mti wa Kihistoria haupo pichani.
Balozi Mulamula (wa pili kutoka kushoto), akipata maelezo ya Mchoro wa maisha ya Binadamu wa Kwanza iliyopo mbele yao kutoka kwa Mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bi. Agnes Gidna (wa kwanza kulia).
Bi. Agnes Gidna akiendelea kuelezea michoro ya mapangoni kwa Balozi Mulamula (kushoto)
Balozi Mulamula akieendelea na ziara yake na kujionea mambo mbalimbali yaliyopo katika Jumba la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam
Balozi Mulamula akiwa kwenye moja ya sehemu maalumu kwa ajili ya  simulizi za Hadithi za watoto wadogo. 
Balozi Mulamula (kushoto) wakizungumza na Bw. Bufure mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye Jumba la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni na tayari kwaajili ya kuendelea na majukumu mengine ya kitaifa.

Picha na Reginald Philip.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top