Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa Jana alitoa shilingi milioni mbili kwa
wahanga waliookolewa katika mgodi wa Nyangalata wanaopatiwa matibabu
katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga.
Akikabidhi
fedha hizo kwa wahanga hao, Lowassa alisema ametoa fedha hizo kama
msaada ili ziwasaidie kwa matibabu kwa muda wote watakapokuwa
hospitalini hapo, ambapo kila mmoja amepatiwa shilingi laki tano.
Mmoja
wa wahanga hao, Joseph Burule alisema kitendo cha Lowassa kuwatembelea
hospitalini hapo kimewapa faraja kubwa, kwani tangu waokolewe na kuanza
kupatiwa matibabu hakuna kiongozi mkubwa aliyefika kuwajulia hali pamoja
na kuwapa pole.
Burule
alisema kitendo hicho kinatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi
pindi linapotokea jambo la kusikitisha kama hilo, na kusema kuwa fedha
hizo zitawasaidia kujikimu hospitalini hapo.
Kwa
upande wake Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga kupitia CHADEMA
Salome Makamba aliwaambia wananchi waliojitoza kumsabahi Lowassa kuwa,
Lowassa amekuja kuwapa pole wahanga hao na hakuja kwa masuala ya
kisiasa.
Novemba
15, 2015 wahanga 5 kati ya 6 waliofukiwa na kifusi katika machimbo ya
nyangalata wilayani kahama waliokolewa wakiwa hai baada ya kukaa ndani
ya mashimo kwa siku 41, ambapo juzi mmoja kati yao alifariki dunia.
This post was written by: Author Name
Your description comes here!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Filed Under:
UKAWA
on Tuesday, November 24, 2015
Post a Comment