Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu amesema anatilia shaka hatua ya Taasisi muhimu kama Bunge kukusanya michango kutoka kwa Taasisi za umma ili kuendeshea shughuli zake, ikiwamo hafla ya uzinduzi wa Bunge mjini Dodoma.
Aidha,
Profesa Baregu ameshangazwa na hatua ya Rais John Magufuli kupokea
fedha hizo na kuzibariki kutumika katika kununulia vitanda katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili bila kuhoji malengo na msingi wa mhimili
huo wa kutunga sheria kuchangiwa fedha hatua ambayo msomi huyo amedai
kuwa ni kumwingiza Rais kwenye mtego wa ufisadi wa kimfumo.
“Bunge
ni taasisi nyeti sana kuruhusu kuchangiwa pesa na watu au taasisi
ambazo linapaswa kuzisimamia. Mara kadhaa wakuu wa mashirika haya
hutakiwa kuhojiwa ikiwemo kuwasilisha matumizi yao mbele ya Kamati za
Bunge; Je, kweli Bunge litakuwa na nguvu ya kuzisimamia endapo linapokea
michango kutoka kwenye Taasisi hizo?” amehoji Profesa Baregu.
Profesa
Baregu ameelezea kitendo cha Bunge kukusanya michango kwa ajili ya
hafla kuwa ni ufisadi wa kimfumo ambao haustahili kuvumiliwa.
Aidha msomi huyo amesema anategemea kuwa kwa umakini alionao Rais Magufuli hatalifimbia macho hili na atawataka Bunge wajieleze ni kwa namna gani wameingia kwenye ufisadi huu wa mfumo na ikiwezekana kuwachukulia hatua wote waliohusika.
Aidha msomi huyo amesema anategemea kuwa kwa umakini alionao Rais Magufuli hatalifimbia macho hili na atawataka Bunge wajieleze ni kwa namna gani wameingia kwenye ufisadi huu wa mfumo na ikiwezekana kuwachukulia hatua wote waliohusika.
Post a Comment