Taarifa nilizozipata zinadai kuna mvutano mkubwa ndani ya UKAWA kuhusu
mstakabali wa UKAWA kwenye bunge la 11 ambalo liko mbioni kuanza Jumanne
ijayo.
Taarifa inasema kuna kundi la viongozi na baadhi ya wabunge wa CHADEMA wanadai ni lazima wahudhurie kikao hiki ambacho wanadai ni muhimu kwa mstakabali wa Kambi ya Upinzani katika maisha ya bunge la 11 kwa sababu kinaenda kumchagua Spika, kuthibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu na uchaguzi wa Naibu Spika.
Kundi lingine la wabunge na baadhi ya viongozi wa UKAWA hasa CUF wanadai kufanya hivyo watakuwa wana legitimise, legalise and justifying the outcome of General Election in Tanzania and Zanzibar. Hawawezi kuanza kuisimamia na kuishauri serikali ambayo wanadhani ni illegitimate and illegal.
Kuna baadhi ya viongozi na wabunge wengine hasa wa CHADEMA mpaka sasa hawana msimamo kamili kwa sababu wanafahamu kama watakataa kuitambua serikali ya Rais Magufuli ina maana hawataingia bungeni wakati Katiba ya nchi katika Ibara ya 71(1)(C) inasema Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake kama atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika.
Kuna habari pia zinasema baadhi ya nchi za Magharibi zimeridhia Uchaguzi wa Zanzibar urudiwe tena. Uamuzi huu unawaweka UKAWA na hasa CUF katika wakati mgumu kutokana na msimamo wao.

Post a Comment