TIKETI
za mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia chini Urusi
mwaka 2018 kati ya Tanzania dhidi ya Algeria ziataanza kuuzwa kesho
Ijumaa katika vituo 10 viliyopo jijini Dar es salaam.
Magari
maalumu yenye stika yataanza kuuza tiketi hizo za mchezo kesho saa 2
kamili asubuhi mpaka saa 12 jioni, ambapo tiketi zinauzwa kwa shilingi
elfu tano (5,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani na rangi ya
machungwa, na elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C.
Vituo
vitakavyotumika kuuza tiketi hizo ni ofisi za TFF – Karume, Buguruni –
Oilcom, Mbagala – Darlive, Mnazi Mmoja, Luther House – Posta, Big Bone –
Msimbazi, Ubungo – Oilcom, Makumbusho – Stand ya Daladala, Uwanja wa
Uhuru.
TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
TFF inawaomba wadau, washabiki na watanzania kujitokeza kwa wingi kununua tiketi za mchezo huo katika magari maalumu yatakayokuwepo kwenye vituo vilivyotajwa, ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Wakati
huo huo Ubalozi wa Algeria nchini Tanzania, umewataka waandishi wa
habari wanaotrajia kwenda kuripoti mchezo wa marudiano jijini Algiers
siku ya jumanne, kuwasilisha maelezo ya chombo wanachofanyia kazi pamoja
na vifaa watakavyovitumia kwenye mchezo huo (camera, vinasa sauti)
kuwasilisha maelezo hayo leo Alhamsi kabla ya saa 9 mchana katika ofisi
za Ubalozi huo kwa ajili ya kupatiwa Accreditation za kufanyia kazi.
Wakati huo huo: Taifa
Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager imerejea jana
jioni ikitokea chini Afrika Kusini ilipokuwa imeweka kambi ya siku kumi,
ambapo leo jioni itafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam.
Kikosi
cha Taifa Stars kinachonolewa na kocha mzalendo Charles Boniface
Mkwasa, kimefikia katika hoteli ya Serena iliyopo eneo la Posta, na leo
jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Washambuliaji
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya
Congo DR wameungana kambini na wachezaji wenzao jana na kufanya kikosi
cha Stars kukamilika kwa maandalizi ya mwisho.
Wapinzani
wa Taifa Stars, timu ya Taifa ya Algeria wanatarajiwa kuwasili leo saa
12 jioni nchini kwa usafiri wa ndege binafsi, na kufikia katika hoteli
ya Kilimanjaro Kempsink (Hyatt) ambapo kesho jioni Ijumaa watafanya
mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es slaam.
Wakati
huo huo waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Mali, mwamuzi wa kati Keita
Mahamadou, Diarra Bala, Niare Drissa Kamory na mwamuzi wa akiba
Coulibaly Harouna tayari wameshawasili nchini leo asubuhi, huku
mtathimini wa waamuzi Attama Ibrahim Boureima kutoka nchini Niger
alishawasili nchini tangu juzi usiku.
Kamisaa
wa mchezo huo Mukuna Wilfred kutoka nchini Zimbambwe anawasili nchini
leo mchana kwa shirika la ndege la Afrika Kusini (South Africa Airways)
SOURCE:BIN ZUBERY
Post a Comment