Msimamizi
wa Uchaguzi wa nafasi ya Meya ndani ya chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Edward Makabayo akizungumza jambo wakati wa
kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Baadhi ya Madiwani walioshiriki zoezi la kumpata Meya wa manispaa ya Moshi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Meya
wa Manispaa ya Moshi aliyemaliza muda wake na Mbunge wa sasa wa jimbo la
Moshi mjini,Jafary Michael akizungumza katika kikao hicho
kilichofanyika Hotel ya Umoja.
Madiwani wakimsikiliza Mbunge Michael kwa makini .
Katibu wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Basil Lema akizungumza katika kikao hicho.
Waliokuwa
washindani katika nafasi ya kuwania kuteuliwa na Chadema nafasi ya Meya
wa manispaa ya Moshi,Francis Shio (kushoto) akimpongeza Raymond Mboya
baada ya kutangazwa mshindi kwa kupata kura 16 dhidi ya kura 10 za Shio
.
Madiwani wakimpongeza Ray Mboya baada ya kutangazwa mshindi.
Raymond
Mboya ambaye pia ni diwani wa kata ya Longuo akizungumza mara baada ya
kutangazwa mshindi wa nafasi ya kuteuliwa na Chadema kupeperusha bendera
katika nafasi ya kugombea kuwa Meya wa manispaa ya Moshi.
aliyekuwa
akigombea nafasi ya Meya ,Francis Shio akizungumza mara baada ya
kushindwa na Ray Mboya huku akiwataka madiwani kuungana kufanya kazi ya
ahadi walizotoa kwa wananchi.
Mshindi wa nafasi ya Naibu Meya ,Peter Minja akishukuru mbele ya madiwani waliompigia kura na kufanikiwa kushika nafasi hiyo.
aliyekuwa
akigombea nafasi ya Naibu Meya ,Jomba Koi na kushindwa na Peter Minja
akizungumza katika kikao hicho akitoa ahadi ya kushirikiana na Meya
aliyechaguliwa.
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa chadema manispaa yaMoshi,Ally Mwamba akizungumza jambo katika kikao hicho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Post a Comment