Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

SIMBA KIBOKO MIEZI 17 MAKOCHA WANNE LAKINI HANS POPPE ASEMA HAWAYUMBISHWI NA WANAOWABEZA

Siku chache baada ya kumtimua kazi aliyekua kocha wao mkuu Dylan Kerr mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya simba Zacharia Hans Poppe amesema hawayumbishwi na lawama za baadhi ya wanachama wao kwa kuwa wanachohitaji ni kutimiza malengo yao
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe
Akizungumza na East Africa Radio Poppe amesema kuwa wameamua kumfuta kazi kocha huyo baada ya kugundua ameshindwa kuwajenga wachezaji wake tofauti na ilivyo sasa chini ya kocha Jackson Mayanja.
Poppe amesema walikua wakimshauri kerr juu ya stamina ya wachezaji wao kuwa mbovu lakini hakuwa msikivu hali iliyopelekea kupoteza imani nae.
Katika hatua nyingine Hans Poppe amesema ni jambo la kawaida kwa kocha kushindwa kazi kwenye timu yake hata kama ni bora mfano mzuri ni kwa Jose Mourinho na Luis Van Gaal ambao katika hali ofauti wameshindwa kuonyesha ubora wao ndani ya Chelsea na Manchester united.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top