Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MNYAMA KAKAKUONA AMEONOKANA KWA MARA YA KWANZA KWENYE HIFADHI YA TAIFA YA KITULO

Mnyama aina ya Kakakuona akiwa ndani ya Hifadhi ya Kitulo

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo, Rimus Mkongwe akizungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) walipomtembelea ofisini kwake hivi karibuni.


MNYAMA ambaye huo anaonekana kwa nadra maeneo mengi nchini na baada ya kuonekana hua na ujumbe pamoja na utabiri katika jamii ameonekana kwa mara ya kwanza katika Hifadhi ya Taifa ya Kitulo tangu kuanzishwa.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo, Rimus Mkongwe alithibitisha kuonekana kwa mnyama huyo na kuongeza kuwa alikutwa na askari wa Hifadhi walipokuwa wakifanya doria ndani ya hifadhi ambapo walimuona maeneo ya Mwakipembwa katika uwanda wa Nyasi.

Alisema walishindwa kupata ujumbe au utabiri wake kutokana na Askari hao kutokuwa na mahitaji muhimu ambayo Mnyama huyo anapaswa kupewa ili atoe utabiri wake ama ujumbe anaokuwa nao.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na Panga, Mkuki na Unga na kuongeza kuwa Mnyama huyo bado yuko ndani ya hifadhi na atahifadhiwa kwa ajili ya watu wanaotaka kumuona hivyo kuongeza kivutio ndani ya Hifadhi.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top