Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

MUENDELEZO WA HABARI: WAZIRI WA ELIMU ASIMAMISHA VIGOGO WANNE BODI YA MIKOPO

Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako amewasitishia mikataba Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mikopo (HESLB) na Wakurugenzi wengine watatu kutokana na utendaji mbovu katika kuendesha bodi hiyo.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo na wenzake watatu kwa uzembe na ubadhirifu wa fedha.

........................................................

Waziri wa Elimu Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesitisha mkataba wa kazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikop George Nyatenga (Pichani).

Pia amewasimamisha kazi wakurugezi watatu wa Bodi hiyo ambao ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yusufu Kisare, Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, Juma Chagonja na Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo kwa utendaji usioridhisha, Prof Ndalichako pia ameagiza kufanyike uhakiki wa maelezo na nyaraka zilizowasiliwa na Bodi ya Mikopo pamoja na kufanya ukaguzi maalum kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi sasa. ============ Update
Mkurugenzi Mkuu wa Mikopo ya wanafunzi asimamishwa kazi, wengine ni Mkurugenzi wa Urejeshaji wa Mikopo, Mkurugenzi Upangaji na Utoaji wa Mikopo.

Mkataba wa Mkurugenzi Mtendaji HESLB umesitishwa.

Waliosimamishwa ni Mhasibu Mkuu, Mkurugenzi wa Utoaji Mikopo Laizer na Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo, wamesimamishwa kupisha uchunguzi.

Amewateua wafuatao ku Kaimu nafasi; Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mteule ni Bw. Jerry Sabi kutoka Mzumbe University na Kaimu Mhasibu Mkuu mteule ni Bw. Daniel Mafie kutoka NECTA
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top