Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne ambao ni Elizabeth Kitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera

post-feature-image 
Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane akizungumza na waandishi wa Habari 
--  
WAZIRI wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane amewasimamisha kazi wakurugenzi wa nne ambao ni Elizabeth Kitundu wa Halmashauri za Misenyi mkaoni Kagera,

   Ally Kisengi wa Halmashauri ya Nanyumbu mkaoni Mtwara, Abdalla Mfaume wa Halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita,  baada ya kubainika wakurugenzi hao  wametenda kosa la kuwahonga wakaguzi wa fedha kutoka katika ofisi ya Mkaguzi mkuu wa  Hesabu za  serikali (CAG) ili wapewe hati  safi huku Halmashauri hizi zikiwa na ufisadi .

   Pia, Waziri Simbachawene   amemsimamisha kazi  mkurugenzi Halmashauri ya  Tunduma Mkoani  Mbeya Bi Halima Ajali  ili kupisha uchunguzi kutokana matumizi mabaya ya madaraka.

  Hata hivyo Waziri Simbachawane pia ameziagiza mamlaka husika kuwasimisha kazi watendaji wa ofisi ya mkaguzi wa Hesabu za Serikali nchini,CAG  waliohusika kupokea rushwa kutoka kwa wakurugenzi hao ili watoe  hati safi kwenye Halmashauri hizo huku zikiwa na ubadilifu wa fedha za Umma.

Akizungumza na waandishi wa habari mda huu Jijini Dar es Salaam,Waziri Simbachawene amesema Wakurugenzi hao wamegundulika  baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na wizara yake,

Waziri Simbachawene ameyataja makosa yao kila mmoja wao ambapo amesema Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misenyi, Bi Chitundu ametenda ametanda kosa  baada ya kumwagiza  mweka hazina wake Majaliwa Bikwato atoe rushwa ya Milioni tatu kwa maafisa ya (CAG) kwa lengo la kuficha kasoro walizoziabini katika ukaguzi huo ,
Ambapo Maafisa  hao wa CAG waliopeka pesa hizo ni Stevin Buawa,John Elias pamoja na Kilembi Mkole,

Waziri Simbachawene amesema Katika Halmashauri ya Nanyumbu ambapo ameidai  tarehe 26 Juni 2015 mkurugenzi wake bwana Kasengi pamoja na mweka hazina Pasco Malowo na mwasibu Emmanuel Mugesa wamlimkabidhi fedha ya Milioni 3 na laki tano  afisa wa CAG ambapo afisa huyo alipokea  pesa hizo kwaniaba ya wenzake kwa lengo la kutoa hati safi,

Sanjari  na huyo pia  Waziri Simbachawene amesema  hata katika Halmashauri ya  Mbogwe mkoani Geita ambapo amedai  mwezi Novemba mwaka jana , Mkurugenzi wa Halmahsauri hiyo Abdalla Mfaume na mweka hazina wake wamliwapat ia fedha maafisa wakaguzi wa C AG ambao walipokea rushwa ya milioni 16 ili wafiche ufisadi walioubaini,

Hata hivyo Simachawene amesema katika Halmashauri hiyo pia kumegundulika kuwepo na ufisadi mkubwa ukiwemo malipo ya mishahara hewa pamoja na malipo ya milioni 200 yaliotolewa pasipo kuwa na Stakabadhi ,

Aidha,Waziri Simbachawene amesema katika wilaya hiyo  ambapo mkaguzi wa mkoa wa Geita alipewa Rushwa kutoka kwa  viongozi wa wilaya hiyo ili kuficha ufisadi wa milioni 90 ambazo zilitengwa kwa ajili ya kununulia dawa.

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amesema  Kwa mamlaka aliyekuwa nayo amemasiamisha  kazi pia mkurugenzi wa Mji wa Tunduma Bi Halima Ajali baada ya kubainika kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo.

Amesema Mkurugenzi huyo alikuwa anawatumia watoto wake kwenye shughuli za Halmashauri huku akiwalipa  pesa pamoja na kuikosesha mapato Halmashauri hiyo yaliyotokana na  Ushuru wa Magari kwenye Mpaka wa Tunduma,
Vilevile waziri Simbachawene amemteua  Erick Mpunda kukaimu nafasi ya mkurugenzi huyo ambapo Mapunda kabla ya kuteuliwa kwake hapo alikuwa Mkuu wa Rasilimali watu wmkoani Mbeya.

Waziri Simbachawene amemuagiza Katibu kongozi kuwasimamisha watendaji wote ambao walihusika na rushwa hizo kwenye ofisi ya CAG  kwa madai kuwa wapo kwenye Mamlaka yake,
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top