Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

BUNGE SPORTS CLUB NA BARAZA LA WAWAKILISHI HAKUNA MBABE,ZATOKA SARE YA BAO 1-1Timu ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge Sports Club usiku wa leo Aprili 26.2016 imeweza kutoka sare ya bao 1-1, dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Unguja na kushuhudiwa na watu mbalimbali.
Mchezo huo wa aina yake na wa kipekee kwa kikosi hicho cha Bunge Sports Club kiliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia wakati wote ambapo waliweza kupata bao lao la kuongoza ndani ya dakika 22 ya mchezo katika kipindi cha kwanza bao safi lililofungwa kwa kushuti la nje ya 18 na kuwaacha Wachezaji wa Baraza la Wawakilishi wasijue la kufanya.
Bao hilo la Bunge Sports Club ambalo lilikuwa la ushindi lilidumu hadi kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 67, Timu ya Baraza la Wawakilishi ilifanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo kuwa 1-1. Bao hilo lilipachikwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hasa mvua kiasi cha kuwapoteza vibaya wachezaji wa timu ya Bunge ambao walicheza katika mazingira magumu sana.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamoto alibainisha kuwa kikosi chake kilicheza soka safi na wataendelea kukiimalisha kwani wanaamini mpira ni ajira ambapo pia alieleza kuwa bila washindani wao ‘kuwachomekea’ wanahakika wangefanya vizuri zaidi n ahata kuibuka na mabao mengi.
Kwa upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid alizipongeza timu zote mbili na kuzitaka kuendelea kudumisha michezo na suala la Muungano kwa ujumla kwani wanahakika kupitia michezo suala hilo litaenziwa kwa miaka yote.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh. January Makamba alibainisha kuwa wataendelea kuulinda Muungano huku akiwataka Watanzania kuishi kwa misingi ya Amani na utulivu kwa kipindi chote ambapo pia alieleza kuwa suala la Michezo litaendelea kuwapo ilikuongeza mshikamano kwa watu wote.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
DSC_2098 DSC_2099Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akitoa maelezo kwa kikosi hicho cha Bunge muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wao huo dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amaan,
DSC_2285Waziri wa Kilimo, Mfugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na mmoja wa wachezaji wa Baraza la Wawakilishi
DSC_2282
Mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi ambaye pia analiwakilisha Jimbo la Tunguu, Mh. Simai Mohamed Said akijadiliana jambo na ,Mwakilishi wa Rahaleo (CCM), Mh. Nasasor Salum Al Jazeera wakati wa mchezo huo maalum dhidi ya timu ya Bunge.
DSC_2150
Timu zikiingia uwanjani
DSC_2151 DSC_2157 DSC_2160 DSC_2162
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mechi
DSC_2169 DSC_2187
DSC_2190 DSC_2197
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
DSC_2197
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
DSC_2202 DSC_2206
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya mchezo huo kuanza...
DSC_2247
Mchezo ukiendelea katika uwanja huo wa Amaan
DSC_2253 DSC_2255
Mashabiki wakifuatilia mchezo huo
DSC_2258 DSC_2259Viongozi wakiwa katikajukwaa maalum la wageni waalikwa.
DSC_2261 DSC_2267 DSC_2271 DSC_2273
Kikosi cha Bunge kikitoka katika vyumba vya kupumzikia kuendelea na kipindi cha pili
DSC_2294 DSC_2296
Viongozi wa timu wakihamasisha timu yao hiyo ya Bunge...
DSC_2305
Viongozi wa timu wakiwa hawaamini baada ya Baraza la Wawakilishi kusawazisha bao hilo na kuwa 1-1...
DSC_2307
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi waliokuwa wapo mapumziko wakifurahia baada ya kusawazisha bao hilo
DSC_2326 DSC_2339Kikosi cha Bunge mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo
nightofhope17DSC_2345DSC_2348 DSC_2352
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza baada ya mchezo huo
DSC_2357
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akizungumza mara baada ya mchezo huo
maxresdefault
Kikosi cha Bunge kikiomba dua mara baaa ya mchezo huo...
DSC_2360Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge (wa pili aliyesimama nyuma) akipata picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliojitokeza katika mchezo huo wa kuimalisha Muungano.
DSC_2371Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba wakipata picha pamoja na Vijana wa Visiwani Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog)
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top