Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

LADY JAYDEE ATOA UJUMBE HUU BAADA YA MAMBO YOTE YALIOTOKEA JUU YAKE


Msani Lady jaydee ambaye anatarajia kufanya onyesho kubwa mwishoni mwa wiki hii, amesema kuwa mafanikio yake makubwa aliyonayo kwenye muziki, yametokana na nidhamu yake kwenye muziki, ambao anauona ni sehemu ya maisha yake.

Jay dee ameyasema hayo alipokuwa akiongea East Africa Televishion, na kusema kuwa muziki ni kila kitu kwake, na hajioni yeye bila muziki.
"Mafanikio yangu mpaka kufika hapa naweza nikasema ni nidhamu niliyonayo kwenye kazi yangu, nauheshimu sana muziki, kwani ni kila kitu kwangu, sijioni mimi bila muziki, hivyo nauthamini sana", alisikika Lady jay dee akisema.
Jay dee ambaye kwa muda alikuwa kimya kwenye muziki na kuibuka na wimbo wa NdiNdiNdi ambao umepokelewa vizuri, amesema hakutarajia kama NdiNdiNdi ungekuwa wimbo mkubwa, kwani hakuwa kabisa na hisia za kutoa kazi yoyote kwa muda huu.
"Unajua baada ya kukaa kimya, sikuwa na hisia ya kuandika wimbo wowote, nikakaa na watu Seven, akaandika, na kuna mtu mwingine kutoka Uganda nae akaandika, lakini waliandika mashairi ambayo walijua nitauvaa uhusika ipasavyo, zikaandikwa na nyingine lakini NdiNdiNdi ndo ikapitishwa itoke, hata sikufikiria ingekuwa kubwa, lakini nashukuru watu wameipokea vizuri sana", alisema jay dee.
Pamoja na hayo Jaydee ambaye amejielezea yeye ni mwanamke mpole lakini ana hasira pale anapokosewa, amewataka mashabiki wake wasiwe na wasi wasi na wasiumizwe na lolote, kwani komando wao yupo vitani anapigana.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top