1. Mara kwa mara wanakuza wigo wa maono yao.
Mbali na ile ndoto waliyokuwa nayo huchukua fursa kwa ukuaji wa uchumi,
ukosefu wa huduma na teknolojia kufungua fursa mbalimbali. Mwenda kwao
hafungwi mlala.
2. Ni watu ambao hufanya kazi kwa malengo.
Hutafuta muda mzuri wa kukaa chini na kutathmini malengo yao, kujikosea
pale walipokosea kisha kuandika mpangokazi wa kuufuata ndani ya muda
fulani ili kukuza biashara au huduma husika.
3. Wanachukua Hatua
Watu hawa wanaelewa kuwa wasipofanya kazi basi ni ngumu kwa wao
kufanikiwa. Hawalalamiki bali hufanya waliwezalo kufanikisha malengo
waliyojiwekea.
4. Hujiweka karibu na wenye manufaa kwao.
Ndugu yangu, Bahari haivukwi kwa kuogelea.
5. Ni wanafunzi maisha yote.
Mara kwa mara hutafuta njia mbalimbali za kujifunza na kujiendeleza
kupitia maisha ya kila siku, toka kwa watu wanaokutana nao na mafunzo
ambayo yanatolewa na Mwalimu Dunia smile emoticon "Chuma hakimegwi - changarawe haitafunwi."
6. Huwatumikia wengine.
Wanaelewa kuwa mafanikio ya biashara au huduma yoyote ni katika kusaidia
watu na kutatua matatizo yao. Hivyo huweka akili zao katika kuhakikisha
wanachofanya kinagusa na kubadilisha maisha ya watu. Hufanya kazi kwa
akili kwamba wao ni watumwa kwa wateja. Kumbuka kuwa Mti haushuliki ila
kwa mti mwingine.
7. Wanafanya kazi kuliko wengine.
Kuna msemo unaosema “Jitihadi haiondoi kuduru ya Mungu.” Watu wengi
hudhani kuwa waliofanikiwa kibiashara ni watu wenye bahati lakini ukweli
ni kwamba hufanya kazi sana Zaidi ya muda wa kawaida, hujitoa na kuvuka
mipaka ili kufanikisha mambo waliyojiwekea hata kama hawana fedha.
8. Huhifadhi chochote kwa Manufaa ya baadae.
Watu hawa hutambua kuwa changamoto ni kwa binadamu hivyo hujipanga kwa
kuweka kiasi kidogo kwa ajili ya baadae kiafya na kimaisha. Ndio maana
nchi za wenzetu wanathamini huduma kama zinazotolewa na mfuko wa jamii, PSPF Tanzania Jua kwamba Mfinyanzi hupika kwa vigae.
9. Hawakubali kushindwa kuwafanye wasifike mbali.
Wakati wengine wanakata tamaa pale wanaposhindwa wao wana#InukaEndelea na
kujaribu vitu vipya. Wanaelewa kuwa mafanikio huhitaji majaribio na
katika majaribio zimefichwa changamoto mbalimbali. Usisahau kuwa Siku
njema ni zawadi ya msafiri.
10. Ahangaikaye sana na Jua ajua.
CHANZO:MPOTO
Post a Comment