Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima
ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika
Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Katika tukio hilo Dk. Tulia Ackson
alichangia kiasi cha shilingi milioni moja.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu (kushoto), Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kulia) na Miss
Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (katikati) wakiosha moja ya magari ya
wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima
ya afya waandishi wa habari nchini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kulia) akiosha gari na Miss Tanzania 2014/15, Lilian
Kamazima (kushoto) kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya
waandishi wa habari nchini. Katika tukio hilo Dk. Hamisi Kigwangalla
alichangia shilingi milioni moja.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiosha gari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo
lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu (kulia) akiosha moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono
waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika
jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza
kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari
‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.
Tulia Ackson Mwansasu na Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya
Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson
(katikati). Katika zoezi hilo Ngeleja alichangia shilingi laki moja huku
timu ya bunge ikichangia shs milioni moja.
Mwenyekiti
wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For
Health’, Benjamin Thompson (katikati) akizungumza katika zoezi la kuosha
magari kwenye kampeni maalumu ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari
‘Media Car Wash For Health’ ikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa
ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia
Ackson na Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (kushoto).
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu (kulia) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa
Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika
Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Dk. Tulia alichangia shs milioni tano.
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson
Mwansasu (kushoto) akiosha moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono
waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya
kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika
jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mmoja
wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na
wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya
waandishi wa habari nchini.
Mmoja
wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na
wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya
waandishi wa habari nchini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (katikati) akimkabidhi hudi ya shs milioni moja Mwenyekiti
wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For
Health’, Benjamin Thompson (kushoto) kwa ajili ya kuchangia fedha
kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni Mratibu wa
zoezi hilo.
Miss
Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na
Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani
(kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo. NHIF waliosha
gari lao kwa shs 100,000/-.
…………………………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Naibu
Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya kuchangia waandishi
wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media Car Wash For
Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambapo
amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha ya waandishi wa
habari.
“Kuna
umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani wamekuwa na
mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na kuhamasisha amani ya
nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi 5,000,000 ili iweze
kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia.
Licha
ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya magari ya
waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo ambapo kila
mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 ambazo moja kwa
moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya waandishi wa habari kwa
kuwakatia Bima ya Afya.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 1,000,000/= ambayo
nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze kukatiwa Bima ya
Afya.
Lengo
la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo
zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya waandishi wa habari 1000 hapa
nchini. Aidha harambee hii ni ya pili, harambee nyingine kama hii
ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na
kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia kugharamia
matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi
kirefu.
Post a Comment