Chelsea wanajiandaa kuingia katika mbio za kumwania kiungo wa Roma Axel Witsel, 27, ambaye yuko Ufaransa na timu yake ya taifa ya Ubelgiji katika Euro 2016 (Daily Mail),
Barcelona huenda wakamnyatia beki wa Arsenal Hector Bellerin, 21,
baada ya Dani Alves kuondona Barca na kwenda Juventus (London Evening
Standard),
Crystal Palace wamekubaliana ada ya uhamisho ya pauni milioni
31.6 ya kumsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Mitchy Batshuayi, 22,
anayechezea Marseille (Guardian),
Manchester City huenda wakawazidi
kete Manchester United na Benfica katika kumsajili winga Marlos Moreno,
19, anayeichezea Atletic Nacional ya Colombia kwa pauni milioni 8 (Daily
Mail),
Real Madrid wanapanga kumtoa mshambuliaji wake Jese, 23, kwa
mkopo msimu ujao, licha ya mchezaji huyo kusakwa na Chelsea na
Manchester United kwa mkataba wa kudumu (AS)
, meneja wa Hull City Steve
Bruce anafikiria kumsajili mshambuliaji kutoka Paraguay anayecheza
Augsburg Raul Bobadilla, 29, anayedhaniwa kuwa na thamani ya pauni
milioni 5 (Daily Mirror)
, Leicester City wapo kwenye mazungumzo ya
kumsajili kiungo Nampalys Mendy, 24, kwa pauni milioni 13, kutoka Nice
(Leicester Mercury),
Zlatan Ibrahimovic, 34, atafanya vipimo vya afya
Old Trafford wiki ijayo kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja (Sky
Sports),
beki wa Chelsea Baba Rahman, 21, anasakwa na Lazio ambao tayari
wametoa dau la pauni milioni 13 kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa
Ghana aliyenunuliwa na Chelsea msimu uliopita kwa pauni milioni 21.7
(Daily Mirror),
Napoli wamekubaliana maslahi binafsi na Hector Herrera,
26, anayesakwa na Liverpool, lakini klabu hiyo ya Italia bado
haijakubaliana na Porto ada ya uhamisho wa kiungo huyo (Tutto Mercatto),
Arsenal wamepanda dau kumtaka mshambuliaji Gabriel Barbosa, 19, ambaye
kifungu chake cha uhamisho ni pauni milioni 40, katika klabu yake ya
Santos ya Brazil (ESPN Brazil),
meneja wa Everton Ronald Koeman
anajiandaa kumsajili kipa Maarten Stekelenburg, 33, ambaye alikuwa
Southampton msimu uliopita kwa mkopo akitokea Fulham (Liverpool Echo
CHANZO:Salim Kikeke
Post a Comment