Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

Wasifu wa Teodoro Nguema Obiang Mangue, mtoto wa Rais wa Equatorial Guinea aliyeteuliwa na baba yake mzazi kuwa Makamu wake wa RaisTN
Teodoro Nguema Obiang Mangue akila kiapo kuwa Makamu wa Rais
Ametokea wapi
Teodoro Nguema Obiang Mangue alizaliwa Juni 25 1969; kwa jina jingine anaitwa Teodori au The Play Boy for Life; ni mtoto wa Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Guinea ya Ikweta (Equatorial Guinea) anayeongoza nchi hiyo tangu mwaka 1979, kwa Mke wake wa kwanza Constancia Okomo. Teodoro Nguema Obiang Mangue ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais Jumatano hii na baba yake mzazi. Kabla ya hapo Teodoro aliwahi kuwa Waziri wa kilimo na Misitu nchini humo kipindi cha utawala wa baba yake kabla hajateuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Pili anayehusika na Ulinzi na Usalama Mei 2012, mpaka Juni 2016  alipoteuliwa kuwa Makamu wa Rais, akijikita hasa katika mambo yahusuyo Ulinzi na Usalama wa nchi hiyo.
Elimu
Nguema Obiang alisoma l’Ecole des Roches iliyopo  Normandy, hii ni shule ya binafsi ya gharama za juu nchini Ufaransa, na vile vile amesoma kwa miezi mitano katika chuo cha Pepperdine huko Malibu lakini kwa mujibu wa gazeti la THE TIMES, alimaliza masoma yake ya shahada katika Chuo hicho.
Maisha
10
Alipokuwa Waziri wa Kilimo na Misitu, Nguema alilipwa kiasi cha paundi za Uingereza 2,700, sawa na shilingi milioni nane za Kitanzania kwa mwezi. Anapenda sana Rap na Hip Hop na ni meneja wa muziki wa Rap. Nguema ni mtu wa starehe, anapenda magari ya aina ya  Lamborghini na safari ndefu za kuendesha gari hasa katika majiji kama Hollywood na Rio de Janeiro. Alishawahi kukodi yatch ya Tatoosh kwa kiasi cha £400,000 (zaidi ya shilingi bilioni 1 za Kitanzania) kwa ajili ya weekend moja kipindi cha Sikukuu ya Christmas aliyotumia akiwa na Mwanamuziki wa Rap toka Marekani, Eve aliyekuwa naye kimapenzi wakati huo. Anamiliki nyumba mbili nchini Afrika Kusini, zenye thamani ya kiasi cha Randi milioni 50,000, 000 na eneo lingine lenye thamani ya dola milioni $31 huko Malibu, California, Marekani. Na vile vile anamiliki Lebo ya kurokodia muziki wa Hip Hop TNO Entertainment.
8
Aliwahi kumiliki magari aina ya Ferrari 7, Bentley 5, Rolls-Royce 4, Lamborghini 2, Porsches 2, Maybachs 2, pamoja na Aston Martin,  ya thamani karibuni dola za Kimarekan milioni 10, na ikambidi akodishe gereji ya ziada kwa ajili ya kuzipaki. Mara nyingi kuvaa viatu sawa na rangi ya gari atakayoendesha siku hiyo.  Mwaka 2008 alimiliki  Buggatti Veyron na Maseratti MC 12, na akaendelea baadae kununua Bugatti Veyron nyingine. Mwaka 2011 alitaka kununua Bugatti Veyron ya tatu lakini gari zote zilitaifishwa na polisi wa Ufaransa wakati wanachunguza juu ya tuhuma za rushwa na mnamo mwaka 2013 vitu vyote viliuzwa kwenye mnada.
4
Maisha yake sana sana yanajumuisha kulala, kufanya manunuzi na kusherehekea kila siku, ‘partying’.  Wageni wa nyumbani kwake ni majumuisho ya ‘Playboy Bunnies’, Wasichana wanalipwa kufurahisha Matajiri ‘Escorts’ , na akiwa Los Angeles Marekani, sehemu yake kubwa ya kustarehe ni Hugh Hefner kwenye Playboy Mansion.
7
Teodoro ni mkusanyaji mzuri wa kumbukumbu za Michael Jackson, anamiliki glovu nyeupe yenye vito vya kung’aa aliyovaa Michael Jackson kwenye matamasha aliyofanya mfalme huyo wa Pop, na imeripotiwa kwamba Teodoro ni rafiki yake dadake Michael Jackson, Janet Jackson.
6
CHANZO:Swahili Times.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top