Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

YANGA KUTOKA WA KIMATAIFA HADI KUWA KLABU TAJIRI AFRIKA

Na Isack (Babati, Manyara)
Nianze kwa kuipongeza timu ya Yanga kwa hatua waliyofika kwenye michuano ya kimataifa (robo fainali) ni hatua kubwa, pongezi hizi ziwafikie viongozi, wachezaji,  wanachama, mashabiki  na watanzania wote kwa ujumla, Yanga inawakilisha Tanzania na ikifanya vizuri Tanzania itakuwa imefanya vizuri, isipofanya vizuri itakuwa Tanzania haijafanya vizuri.
Baada ya utangulizi huo, ninavitu vichache ambavyo nafikiri vitaisaidia timu ya Yanga kutoka ‘wakimataifa’ hadi timu tajiri.
Mpira wa miguu ni biashara inayolipa kupita biashara zote ambazo ni halali hapa duniani kwa sasa. Ni kwa ufahamu wangu mdogo.
Nasema Yanga kutoka wa kimataifa hadi timu tajiri kwa sababu zifuatazo:-
Yanga inamashabiki wengi hapa nchini kuliko timu yeyote ikifuatiwa na Simba kulingana na maeneo mbalimbali ambayo nimeishi hapa Tanzania japo wengine watanibishia. Sipo hapa kwa ajili ya kubishana ila natoa mawazo yangu tu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji pato la Yanga kwa mwaka ni billion 1.5, lakini matumizi ni bilioni 4, bilioni 2.5 anatoa mfukoni kwake.
Kwa mawazo yangu Yanga ni timu tajiri sana kama nitakavyoeleza hapa chini:-
Yanga inamashabiki zaidi ya milioni 10, lakini wanachama sidhani kama wanazidi milioni 2. Ok ni assume wanachama hai ni laki 3 nchi nzima na watakao kuwa hai (kulipia kadi) kwa muda wa miaka 5 ijayo ni 135,100 tu hapa yanga inauwezo wa kupata billion 14.1 (14,100,000,000) kwa mwaka kwa sababu zifuatazo.
NAAINA WA UANACHAMAIDADIADAADA KWA MWEZIADA KWA MWAKA
1Wanachama wa kawaida.100,0002,500250,000,0003,000,000,000
2Wanachama wa kati30,00010,000300,000,0003,600,000,000
3Wanachama (VIP)5,000100,000500,000,0006,000,000,000
4Wanachama wa heshima.100Hawa hawalipi ni kama Mama Fatuma Karume  wengine

Jumla ndogo12,600,000,000
Kwa mawazo yangu Yanga inatakiwa kuwa na aina nne za wanachama kama ilivyo kwenye hili jedwali hapa chini.
Ukijumlisha na billion 1.5 kwa maelezo ya Mwenyekiti ambazo zinapatikana kwa mwaka, jumla kuu ni 14,100,000,000. Na hii inawezekana kabisa, leo hii haiwezakani mwanachama analipa elfu 12 kwa mwaka anakuwa na sauti kwenye timu hii ni ajabu. Wakati wanapendekeza kiwango cha elfu 1 kwa mwezi nadhani dollar moja ilikuwa sawa shilingi elfu 1, leo hii dollar 1 ni sawa na shilingi elfu 2,200 (wastani).
Nimeweka magroup manne ya wanachama ili kutoa hamasa watu wajitoe (wachangie) na kutambua umuhimu wao.
Mfano group na 1 hakuna haja ya kupiga kura, kura wapige kuanzia group no 2. Nina sababu mtu amechangia elfu 30 kwa mwaka na wakati kukodi ukumbi, kuchapisha karatasi za kupigia kura, chakula, ulizi, posho za wasimamizi n.k kwa siku ya kupiga kura ni gharama kubwa sana (mimi nitakuwa kwenye hili group no 1). Wanachama kundi la 3 ni wale marafiki kama Ndama mtoto ya Ng’ombe, David Mosha, Jerry Muro, Wema Sepetu, Waheshimiwa wabunge n.k. kundi la nne ni watu mwenye michango ya muda mrefu kama Mh. Magufuli, Mh. Jakaya Kikwete, Mama Fatuma Karume, Yusuph Manji na wengine ambao siwajui.
Hata uwanjani kuna madaraja mbalimbali, VIP C na B, VIP A iwe kwenye ndege n.k na hii itaongeza hamasa kwa wanachama kutoka daraja moja kwenda jingine.
Kuwa na database ya wanachama ambapo mwanachama asipo lipia computer (system) ina mwalert na asipolipa miezi 3 system inamtoa na inabidi aombe umpya au kulipa fine.
Timu itaweza kuingiza billion 14.1 au zaidi kwa mwaka?
Matumizi ya club
Matumizi ya club kwa mwaka kwa mujibu wa Mwenyeki ni billion 4 tu, na ongeza billion 1 iwe billion 5 kwa mwaka. Club itabaki na billion 9.1 ambazo ni fedha nyingi sana zinaweza kufanya yafuatayo kwa mwaka mmoja.
  1. Club inawezaka kununua maeneo kwenye kanda zote 4 (Kaskazini, Kanda ya ziwa, Kati na Kusini) Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya.
  1. Maeneo ya pembezoni mikoani siyo ghali kama Dar es salaam, club itaweza kuwa na vitega uchumi vya kutosha. Ekari moja mikoani ni wastani wa million 10 x 10 ekari = 100,000,000 kanda zote 4 sawa na million 400,000,000 chenji inabaki billion 8.7 ambayo itatumika kujenga uwanja ambao hauzidi billion 2, kwa viwanja 2 ni sawa na billion 4. Hostels, guest houses nzuri na sehemu za wazi kwa ajili ya sherehe (beach/garden) 2@ billion 2 (Arusha na Mwanza)= 4 billion Hapo ni mwaka wa kwanza, mwaka unaofuata ni Dodoma na Mbeya kwa wastani wa billion 4 @ (uwanja, hostel, quest  house/hotel,  beach/garden).
  1. Mikoani quest/hotel ya billion 2 ni ya kisasa hapo pamoja na ukumbi, swimming pool, garden, sehemu za kufanyia michezo n.k
  1. Kujenga uwanja Dar es salaam hapa ni mwaka wa tatu na wa nne. Billion 9.1 zinatosha kuanza ujenzi uwanja wa kisasa pembeni mwa jiji ambapo mnaweza kununua ekari 10 @ million 40,000,000 = 400,000,000. Billion 8.7 ikatumika kwa ajili ya ujenzi, kwa miaka 2 billioni 16 ni uwanja wa kisasa.
FAIDA
  • Club itakuwa ikisafiri kwenda mikoani inafikia kwenye maeneo yake hakuna gharama za uwanja wa mazoezi, kulala na chakula.
  • Timu ya vijana (Academy) itatumia kituo kimoja kama kambi yake.
  • Fedha za kuendeshea Academy zitapatikana kutokana na vitega uchumi hivyo.
  • Kumbi zitakodishwa, guest wageni mbalimbali watafikia, timu mbalimbali zitakodi uwanja pamoja na hostel.
  • Timu itaongeza ajira kwa wanachama wake kwenye kanda (mfano; Meneja, Mhasibu, ICT Officer, Dereva, Wahudumu, Walizi na Wapishi n.k).
  • Timu inaweza kukopa mkopo mkubwa toka bank kama CRDB, TIB n.k kupitia asset zake.
  • Timu itakuwa inachagua iweke wapi kambi kwenye sehemu tulivu.
  • Timu itajitengemea daima bila kumtegemea mtu/mwanachama yeyote.
  • Timu itakuwa karibu na wanachama wake wa mikoani ambapo wataweza kuteua wenzao wa kuwawakilisha kwenye mkutano mkuu.
  • Timu itavutia wafadhili wengi zaidi
  • Timu itavutia wawekezaji wengi wa ndani na nje.
  • Timu itakuwa na uwezo wa kusajili wachezaji wazuri zaidi.
  • Timu itavutia wachezaji wazuri kutokana na mazingira mazuri.
  • Timu itakuwa na uchumi imara na Manji hataongezea billion 2.5 kwa mwaka.
  • Timu itachangia pato la taifa kwa kulipa kodi, ajira n.k
  • Billion 2.5 anazotoa Manji zitawasaidia wananchi wa kata ya Mbagala, kwa miaka 5 Mbagala itakuwa kama Ulaya.
  • Timu itakuwa na uwezo wa kuingiza kipato cha milioni 50 kwa mwezi kwa kila kanda, kanda 4 sawa na million 200 na kwa mwaka billion 2.4 nje na wanachama.
Hizo ni baadhi ya faida ambazo inaweza kuzipata kwa mawazo yangu.
Faida zipo nyingi sana lakini sitaweza kuzitaja zote, hizo ni baadhi tu.
Hitimisho
Timu ianjiri Marketing Officer kazi yake aitangaze na kuishauri vizuri timu ili kuuza bidhaa (products) mbalimbali, ICT Officer kwa ajili ya ku-update website ambapo itatumika ku-update taarifa mbalimbali kama (historia ya timu, majina ya viongozi, wachezaji, vikombe n.k) na kuwa timu ya kisasa, watu watatumia kutangazia biashara zao.
Kwa kuanzia mtaji mnaweza kukopa bank CRDB, TIB n,k hata billion 2 tu baada ya kuandika proposal/andiko nzuri  ambapo mtaweza kuzishawishi bank. Naamini wanachama wakihamasishwa vizuri wanaweza kuzilipa kupitia michango yao bila tatizo.
Baada ya miaka mitano Yanga itakuwa mbali sana hapa Afrika.
Mkiyafanya haya Yanga mtakuwa timu Tajiri badala ya ‘wakimataifa’ na inawezekana baada ya miaka 5-8 mtakuwa na ndege yenu na kuwa club ya kwanza Tanzania kuwa ndege.
Yote yawezekana pale mtakapokuwa na mpango mkakati wa muda fupi, kati na mrefu.
Nawatakia mafanikio mema.
0715163816
Babati – Manyara.
Nakala
Wadau wa michezo wote Tanzania.
author

This post was written by: Author Name

Your description comes here!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana
Chediel . Powered by Blogger.
© Copyright Rundugai Blog
Back To Top